• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

COPRA YAKABIDHI MBEGU YA KISASA YA CHOROKO TANI 1.5 MWANZA

Posted on: October 24th, 2025

Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) imekabidhi Mbegu ya kisasa ya Choroko tani moja na nusu kwa Wakulima wa Mkoa wa Mwanza kwa ajili ya kuzitumia katika msimu wa kilimo wa 2025 ambapo zitasaidia kuongeza uzalishaji.

Akiongea katika hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza leo tarehe 24 Oktoba, 2025 Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa huo Mhandisi Chagu Ngh’oma ameishukuru taasisi hiyo na akatoa wito kwao kuwatafutia masoko wakulima ili walime kwa manufaa.


Bwana Ngh’oma amesema choroko kwa kipindi kirefu limekua ni zao la chakula na kidogo biashara hususani katika wilaya za Kwimba na Misungwi ila ujio wa taasisi hiyo na mikakati yake unatarajiwa kuleta manufaa kwa wakulima kuzalisha zaidi na kuuza na hatimaye kukuza hata uchumi wao.

Ameongeza kuwa kwa msimu wa 2024/25 mkoa wa Mwanza ulipanga kupata tani elfu 30 za choroko ila ulipata tani elfu 27 sawa na 73% kutokana na changamoto kadhaa ikiwemo ya mbegu duni ila ujio wa mbegu hiyo ya kisasa utasaidia kufikia malengo kwani wakulima watakua na uhakika wa uzalishaji.


Aidha, amewataka wataalamu kuanzia ngazi za chini (maafisa Ugani) kusimamia ipasavyo ili kufikia malengo yaliyopangwa na kwamba itasaidia pia kuongeza mapato ya halmashauri kutoka kwenye zao hilo huku akibainisha kuwa kwa mwaka 2024/25 Kwimba ilikusanya milioni 300 na Misungwi ikijikusanyia Milioni 70.


Naye, Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Maendeleo ya Mazao ja Viwango COPRA Bi. Pendo Bigambo amesema taasisi hiyo imetoa mbegu hizo ili kuchagiza uzalishaji na amewataka wasimamizi kuzigawa mbegu hizo kwa kufuata muongozo wa mfumo ili kuwa na usawa.

Ameongeza kuwa kwa kanda ya ziwa taasisi hiyo kinara wa usimamizi mifumo ya uzalishaji na usimamizi wa mazao kwa mwaka huu imetoa tani 192 ya mbegu bora za zao hilo ili kusimamia uzalishaji, uchakataji na kwamba itahakikisha mkulima anapata soko la uhakika wa mazao.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti