• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

DC LUDIGIJA ATOA WITO WIZARA YA MIFUGO KUSIMAMIA NA KUFUATILIA DAWA ZA MIFUGO

Posted on: August 6th, 2024

DC LUDIGIJA ATOA WITO WIZARA YA MIFUGO KUSIMAMIA NA KUFUATILIA DAWA ZA MIFUGO


Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija ametoa wito kwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuweka Kitengo maalumu cha ufuatiliaji na usimamizi wa dawa ya mifugo kama ilivyo kwa dawa za binadamu na vipodozi ili kuleta ufanisi katika uuzaji wa dawa za mifugo.

Mhe. Ludigija ametoa wito huo alipotembelea mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi leo Agosti 06, 2024 katika viwanja vya Nyamhongolo yanapofanyika maonesho ya nanenane kwa Kanda ya Ziwa Magaharibi ambapo amewataka wataalamu hao kufikisha ujumbe huo katika ngazi ya juu wa ajili ya utekelezaji.

Mkuu huyo wa Wilaya amesema amekuwa akipokea malalamiko mengi ya wananchi kuhusu uuzwaji wa dawa za mifugo ambazo zimemaliza muda wake na hivyo kupelekea wananchi wengi kukosa imani na dawa hizo mwishowe kupoteza mifugo yao kutokana na magonjwa.

"Nimekutana na changamoto hii, wananchi wengi wanalalamika wanapewa dawa za kuosha ng'ombe ili kuuwa kupe lakini hawaoni magonjwa hayo yakimalizika na Wataalamu wetu wamefuatilia wamegundua dawa wanazouziwa wananchi hao ni feki na zingine zimekwisha muda wa matumizi".Mkuu wa wilaya.

Ni vizuri sasa wadau wetu wa mifugo kushirikiana na kuanza kufuatilia kwa karibu, kupita katika maduka hayo hata kwa kuanza na wale wasambazaji wakubwa ili tuweze kunusuru mifugo ya wafugaji inayokufa kila siku kutokana na kukosa dawa sahihi, ameongeza Mkuu huyo wa Wilaya.

Aidha DC Ludigija amewapongeza wananchi wanaoendelea kutembelea maonesho hayo na kuwataka kutumia elimu ya kilimo wanayoipata kupitia maonesho hayo kujiletea mafanikio lakini pia amewataka wananchu hao kuwapatia pia elimu hiyo wale ambao hawakuapata nafasi ya kutembelea maonesho hayo ili kuleta tija na mageuzi ya kilimo.

Mhe. Ludigija ametembelea maonesho hayo kujionea pia hali ya  maandalizi ya kilele cha nanenane ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda na kutoa maelekezo kadhaa kwa waandaaji wa maonesho hayo ili kuboresha sherehe za kilele hicho.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti