• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Gati la mv Tegemeo lawekewa mkakati wa kuliboresha - Mongella

Posted on: February 6th, 2020

Wananchi  wa Kisiwa cha Maisome na Kaunda watakiwa kuwa wavumilivu kwa changamoto walionayo baada ya gati la kivuko cha mv tegemeo kilichokuwa kikiwaunganisha kukatika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha hivyo serikali inashughulikia harakati za kuwatengenezea  kivuo hicho.

Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella wakati wa ziara yake ya kukagua uharibifu wa miundimbinu mbalimbali ya barabara na madaraja yaliyokatika kutokana na mvua katika wilaya ya Sengerema na  Buchosa.

 Kwa upande wao Wakala wa Ufundi na Umeme ( TEMESA )wameleta mainjinia  kuona kitu gani kinaweza kufanyika kwa haraka ili ushukaji na upandaji kwenye kivuko uwe rahisi na salama.

Pia aliwataka mawakala hao kuhakikisha wanafanya kazi usiku na mchana ili kuondoa changamoto hiyo na kuongeza kuwa itakuwa ni Serikali ya ajabu baada ya kuona changamoto hiyo alafu wakataka kurahisisha mambo,uwekwaji wa ratiba ya kivuko hicho uzingatiwe ili kuwasaidia wananchi.

“Mimi nimekuja nimeona kweli ni changamoto kuna wazee wanasema jambo hilo halijawahi kutokea hivyo tushukuru Mungu kwa baraka ya mvua lakini tuitumie vyema kwa kulima ili kupata mazao mengi na ya kutosha inawezekana anatujaribu ili kuona watu wana bidii gani haya mengine Serikali inayashughulikia ”alisema Mhe. Mongella.

Pia aliwataka TEMESA kujenga banda la watu kusubilia usafiri  na choo hivyo kufikia juni 1 mwaka huu viwe vimejengwa, sambamba na kuweka ratiba ya kivuko inayoeleweka pamoja na gharama za mizigo na nauliu na kuachana na tabia ya kutamka bei pasipo kuwa na mpangilio.

 Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Sengerema Mhe. Dkt. Emmanuel Kipole alisema, kivuko hicho kimekuwa kikitoa huduma katika mikoa miwili kati ya Geita na Mwanza, ila kutokana na changamoto hiyo ratiba imebadilika ya shughuli za usafirishaji wa eneo hilo ambapo kivuko kinatakiwa kusimama kabla ya saa 12 :30 jioni ili wanaichi waweze kupita wakati wa mwanga  ili kuondokana na changamoto wa  uwepo wa wanyama pori kama kiboko na mamba katika eneo.

“Wananchi wanaendelea kutupa ushirikiano pia kwa hii changamoto ya kuwepo kwa wanyama wanaowadhuru taarifa zimefika kwenye kikosi cha wanyama pori watakuja kufanya jukumu lao na kukabiliana na wanyama hao na kuleta amani kwa wananchi”alisema Dkt. Kipole.

Samsoni Nyanda na Marco Lufungulo ni Baadhi ya wakazi wa maeneo hao  walisema kitendo cha gati ilo kuzingirwa na maji baada ya kina kuongezeka kimewajengea hofu kubwa ya kupoteza maisha wakati wanapo kwenda kupata huduma hiyo, pia ikidhaniwa eneo hilo kuwepo wanyama wakali  aina ya viboko na mamba.

Aidha, waliiomba Serikali kuharakisha marekebisho ya gati la kivuko hicho kinachofanya safari zake kati kaunda, maisome na mkoa wa geita kisiwa cha nkome, baada ya kujaa maji kutokana na kina kuongezeka kitendo kinachopelekea kuhatarisha maisha yao.

Kivuko hicho cha mv tegemeo kilizinduliwa na mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  September 26 mwaka 2014.





Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti