• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

HALMASHAURI YA ILEMELA YAPATA HATI SAFI MIAKA 5 MFULULIZO RC MTANDA AIPONGEZA

Posted on: June 26th, 2024

HALMASHAURI YA ILEMELA YAPATA HATI SAFI MIAKA 5 MFULULIZO RC MTANDA AIPONGEZA


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ameipongeza Halmashauri ya Ilemela kwa kupata hati inayoridhisha kutoka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesbu za Serikali (CAG) kwa miaka mitano mfululizo.

“Halmashauri hii imepata hati inayoridhisha kwa miaka mitano mfululizo, mkipata hati hii maana yake ni kwamba hata msimamizi wa Halmashauri na Wilaya kwa ngazi ya Mkoa ni Mkuu wa Mkoa hivyo na Mimi nimepata hati inayoridhisha hongereni sana".  RC Mtanda katika kikao cha Baraza maalumu  la Madiwani kilichojadili taarifa ya CAG ya mwaka wa fedha 2022/2023 kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo mapema leo Juni 26, 2024.

Hata hivyo, Mkuu huyo wa Mkoa amelitaka Baraza la Madiwani kuendelea kusimamia menejimenti ya halmashauri hiyo ili kuhakikisha inaendelea kupata hati inayoridhisha au safi miaka ijayo.

Aidha, RC Mtanda ameipongeza halmashauri hiyo kwa kuwa na hoja chache ambapo jumla walikuwa na hoja 29 za muda mrefu ambapo hoja 21 zilishafungwa na Halmashauri imebaki na hoja 8 za kujibu.

"Nimekuwa nikisikiliza hizi hoja nane na nimeridhika kuwa hoja hizi zitafutwa kwa kuwa mipango ya kuzifuta ipo na inawezekana, ninaiagiza Halmashauri hii kuhakikisha inajibu na kutekeleza kwa wakati hoja zote nane ambazo hazijatekelezwa".Mtanda

Mkuu huyo wa Mkoa ameitaka Halmashauri hiyo kuwasilisha mpango wa utekelezaji wa hoja zilizobaki kwa Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa na namna zitakavyotekelezwa na kuziondoa kabisa ifikapo tarehe 28 mwezi wa sita mwaka huu.

Mhe. Mtanda amesisitiza pia kuhusu ushirikiano baina ya Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Ilemela na Ofisi ya CAG kwa hesabu za mwaka 2023/2024 ili waweze kuondokana na Hoja.

Naye Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo, Mhe. Renatus Murunga ameahidi kutoa ushirikiano na kufanya kazi kwa bidii ikiwemo kuyasimamia maagizo yote yaliyotolewa na Mhe. Mkuu wa Mkoa, aidha amesema yuko tayari kwenda na kasi ya Mkuu huyo wa Mkoa.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti