• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Jaffo afurahishwa kasi ya ujenzi wa Jengo la Utawala Manispaa ya Ilemela

Posted on: October 22nd, 2018


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)Mhe. Suleiman Jaffo amesema ameridhishwa na kasi ya ujenzi inayofanywa na uongozi wa manispaa ya Ilemela.

Mhe. Jaffo ameyasema hayo muda baada ya kutembelea jengo hilo na kulikagua akiwa ameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Dkt. Severine Lalika, Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa hiyo John Wanga, watumishi wa Manispaa ya Ilemela na Mhandisi mshauri  wa Wakala wa majengo Benard Mayemba.

Mhe.Jaffo alimtaka Mkandarasi anayejenga jengo hilo la utawala kuhakikisha kuwa ifikapo Novemba 30 mwaka huu ahakikishe kuwa jengo hilo ambalo ujenzi wake unafanywa na Wakala wa Majengo (TBA) kupitia kikosi chake cha ujenzi cha BRIGADE kama mkandarasi mshauri uwe umekamilika.

“ Kwa kweli nimefurahishwa na kasi inayiofanywa na Mkandarasi anayejenga jengo hili, ukiliangalia limekidhi viwango niwapongeze sana," alisema Mhe.Jaffo.

Alisema Serikali imetoa kiasi cha Sh.  bilioni 38 kwa nchi nzima kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya majengo mbalimbali kwa halmashauri nchini, likiwemo jengo hilo la utawala la manispaa ya Ilemela.


Alimtaka Mkandarasi anayejenga jengo hilo la utawala, ambaye alikuwa amesimama kwa muda kwa sababu ya malipo kuendelea na ujenzi wa jengo hilo na kwamba Serikali italeta fedha za ujenzi wa jengo hilo.

Waziri Jaffo alisema jengo hilo la utawala  litakapokamilika litakuwa ni jengo kubwa na zuri la mfano lililojengwa kwa thamani halisi ya fedha kwa halmashauri zote nchini.

Kwa upande wake Mhandisi mshauri wa Wakala wa majengo Benard Mayemba alimueleza Waziri Jaffo kuwa utekelezaji wa mradi huo kwa sasa umefikia asilimia 35 na kwamba jumla ya wiki 24 zimetumika kwa ajili ya ujenzi kati ya wiki 52 za mkataba wa ujenzi huo.

Alisema hadi sasa TBA imeishapokea toka kwa Mshitiri kwa niaba ya Serikali Manispaa ya Ilemela jumla ya Sh.  996,793,934.50 malipo ambayo yamefanyika kwa awamu moja ambayo yalilipwa mwezi April mwaka huu ambapo utekelezaji wa mradi ulianza rasmi Mei 6 mwaka huu na kwamba kiasi cha Sh.bilioni 3.8 kinatarajiwa kutumika kwenye ujenzi wa jengo hilo la utawala.

Aidha Muyemba alisema kuwa licha ya juhudi zinachukuliwa na manispaa na wakala katika utekelezaji wa mradi huo, bado mradi huo unakabiliwa na changamoto kuu tatu ambazo ni ukosefu wa fedha kutokana na kutegemea ruzuku ya Serikali, upatikanaji duni wa maji kutoka Mamlaka za maji na uhaba wa vifaa vya ujenzi.

“ Kutokana na changamoto ya upatikanaji wa maji, Wakala kwa sasa unanunua maji kwenye ma-bouza na tayari Mshitiri ameishataarifiwa juu ya tatizo hili, ingawa maeneo haya ulipo mradi huu yanakumbwa na tatizo la jumla la uhaba wa maji,” alisema.

Kazi zinazotekelezwa kwenye mradi huo ni kujenga uzio kuzunguka eneo la mradi, kufanya setting ya jengo, kuchimba eneo la kujengea, matayarisho ya kujenga vitako vya nguzo ukuta wa msingi wa jengo na kumwaga zege la jamvi la chini kwa asilimia 100.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti