• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Kivulini Yakabidhi Kompyuta 10 serikalini

Posted on: August 27th, 2019

Shirika   la Kutetea Haki za Wanawake na Watoto (Kivulini) limetoa  msaada wa kompyuta mpakato 10 katika  vitengo maalum  vinashughulikia  masuala ya ukatili wa jinsia kwenye  ofisi  ya mkuu wa mkoa wa Mwanza,  Kamanda wa Polisi mkoa huo,Hospitali ya Rufaa ya mkoa –Sekoutoure na  Wilaya ya Misungwi.

Makabidhiano hayo yalifanyika  kati ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kivulini, Yassin Ally na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Christopher Kadio ambaye  pia aliwakabidhi wakuu wa vitendo husika  na kuwataka kuvitumia kwa malengo yaliyokusudiwa ili  kutekeleza Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto  2017-2022 (MTAKUWWA).

 Akizungumza baada ya makanidhiano hayo, Ally alisema lengo la kutoa msaada wa vifaa hivyo ni kutaka kuimarisha  mfumo wa data-kazi ili kuhifadhi kumbukumbu za vitendo vya ukatili  vinavyotokea ndani ya jamii na kufikia lengo la taifa la kupunguza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Ally alisema  amelazimika kutoa  msaada huo katika idara hizo kwa sababu  katika kufanya  kazi ya mapambano ya kutokomeza vitendo vya ukatili, alibaini kuwapo na changamoto ya watendaji wa Serikali kukosa sehemu salama ya kuweka kumbukumbu zao ambapo   nyingi huandikwa kwenye makaratasi na mara nyingine zinapotea.

“ Vitendo hivi vya ukatili bado ni tatizo kubwa sana, ili kuona ukubwa wake nendeni polisi mkaone mashauri yanayopokelewa lakini mengi yanaishia huko huko katika hatua ya upelelezi  na machache ndio yanafikishwa mahakamani lakini yanayopata mafanikio yanaweza kuwa 20 kati ya 100.

“Ndiyo maana  kama shirika la Kivulini tumeona katika kutimiza malengo yetu tumekuwa tukishirikiana na  polisi, hospitali na Ofisi ya Mkuu wa mkoa , wilaya na idara zake, hivyo tumenunua kompyuta 10 zenye thamani ya Sh milioni 12, namkabidhi Katibu Tawala wa Mkoa ambaye  atazikabidhi kwa wahusika, haiwezekani tukawa tunapamba na jambo huku hakuna sehemu ya kuweka kumbukumbu.

 Ameongeza kuwa watumishi wa Serikali hasa sekta ya afya bado hawapo tayari kujitokeza kutoa ushahidi mahakamani pale wanapohitajika jambo ambalo linaathiri malengo ya kutokomeza vitendo hivyo, vile vile aliwaomba polisi kuongeza jitihada za upelelezi kwani mashauri mengi yanaishia mikononi mwao.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa huo, Christopher  Kadio amesema msaada uliotolewa na Kivulini ni mkubwa ambapo aliwataka wajumbe wa kamati ya ulinzi ya wanawake na watoto ngazi ya mkoa kutekeleza majukumu yao ipasavyo na kuhakikisha wanakomesha vitendo vya ukatili wa ngono, kihisia, kimwili na kiuchumi.

“Hakikisheni sasa mnatanua wigo wa kupambana na vitendo hivi maana  mtoto akishafanyiwa ukatili tayari inaathiri ukuaji na malengo yake, sote tunajua  mpango wa serikali umejikita katika maeneo nane ya kufanyia kazi ikiwamo  kuimarisha uchumi wa kaya, kukomesha mila na desturi mbaya, kuimarisha malezi, kujichukulia sheria, utoaji wa huduma kwa waathirika, kuratibu na kutathimini zoezi hilo.

“Kwa kuwa vitendea kazi vimepatikana, utaratibu  ni kwamba vikao vya mrejesho vitakuwa vikifanyika kwa kila robo ya mwaka ili kuona mafanikio yake kufikia 2022, naomba kila mjumbe wa kamati ya ulinzi wa wanawake na watoto ya mkoa, aone ana wajibu wa kuleta mbinu ya kumaliza tatizo hili,”alisema.

Naye Mwakilishi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Murilo,  Slyvester  Ibrahimu, alisema licha ya kuwapo na mapambano ya vitendo vya ukatili lakini takwimu za makosa yaliyoripotiwa polisi yanaonekana kupanda  tangu 2016 hadi Juni 2019.

Alisema mwaka 2016 makosa ya unyanyasaji na ukatili kwa watoto yalikuwa ni 1165, 2017 yalikuwa 1287, 2018 ilikuwa1683 na  mwaka huu kufikia Juni yameripotiwa 1012.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti