KWA HERI MWENGE WA UHURU MWANZA




Leo tarehe 01 Septemba, 2025 Mwenge wa Uhuru umekabidhiwa Mkoani Geita katika Kata ya Lwezera baada ya kuhitimisha mbio zake Mkoani Mwanza ambapo umetembelea, kukagua, kuweka mawe ya msingi na kuzindua jumla ya miradi 56 yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 100 katika halmashauri 8.

