• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Mafundi simu waonywa kununua simu za wizi

Posted on: April 7th, 2019


Jeshi  la Polisi Mkoa wa Mwanza  limesema tayari limenasa mtandao wa mafundi simu ambao wananunua simu za wizi  zenye thamani kubwa na kwenda kuziuza au kubadilishana na wahalifu wa  nchi jirani na Kenya ambao hukutana mpakani.

Akijibu maswali ya wadau  mbalimbali katika simina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa watoa huduma za mawasiliano nchini, Mussa Zuberi kutoka kitengo cha makosa ya mitandao Mkoa wa Mwanza, alisema mtandao huo umebainika baada ya kuanza kuwakamata mafundi simu na kuwahoji.

 Alisema kwamba baada ya jeshi la polisi kupokea kesi nyingi za upotevu wa simu na kufuatilia ilibainika hupelekwa kwa mafundi simu ambao huziondoa namba ya siri na kubadilisha namba ya utambulisho  yaani IMEI kwa matumizi.

TCRA imeandaa simina kwa wadau mbalimbali  wakiwamo kampuni za mawasiliano Tanzania, viongozi wa umoja wa mafundi simu, waandishi wa habari, viongozi wa dini  na wadau wengine wa sekta hiyo ikiwa  lengo ni kukumbushana taswira ya sheria ya makosaya mitandao ya mwaka 2015 na changamoto zinazojitokeza.


Zuberi alifafanua kwamba  baadhi ya simu zingine ambazo mafundi hao huzinunua huzipeleka mpakani mwaka Kenya na Tanzania na kuziuza au kubadilishana na mafundi wa Kenya jambo ambalo huwafanya polisi kitengo cha  mkoasa  ya mitandao kupata ugumu wa kuzipata kwani huwa hazionekanani katika mfumo wa mtandao.

“Mpaka tunapozungumza  sasa tayari baadhi ya mafundi   wanashikiliwa kwa vitendo hivyo na wametueleza namna biashara hivyo inavyofanyika, wanakwenda kule mpakani Sirari upande wa Tanzania wanakutana na wenzao wa Kenya wanabadilishana au kuuziana hizo simu za wizi, ndio maana mtu anaweza kuleta malalamiko tukashindwa kuipata simu yake.

“Tunapoitafuta kwenya mfumo wa mtandao wetu haipatikani kwani inakuwa nje ya Tanzania lakini mtumiaji yule anapokuja upande huu huwa inasomeka kwa muda na kutoweka sasa inakuwa  vigumu  kuifuatilia kwani tunakuwa mbali na mhalifu.

“Kikubwa tunachowaomba mafundi simu watambua kitendo cha kuanza kuchokonoa simu kwa kufuta namba ya siri iliyowekwa na mhusika sambamba na IMEI ni kosa, kosa la pili ni kuuza mali za wizi, hivyo tumewataka kuacha biashara hiyo na kushirikiana na polisi kuwakamata wale wanaowapelekea simu,”alisema.

Zuberi alisema hivi sasa wanatarajia kukutana na watu wa idara ya uhamiaji kuona namna kufanya ukagazi mpakani Sirari mkoani Mara  katika  mabegi ya abiria na pale wanakuta mtu akiwa na simu nyingi ambazo hazimo katiba maboksi rasmi au kutokuwa na stakabadhi za manunuzi zinapaswa kushikiliwa kwa mahojiano zaidi.

Hata hivyo alisema baadhi ya watu walioibiwa simu zao hukata tamaa pale anapotakiwa kutoa ushirikiano  ambapo alitoa wito kwa jamii kuwa waangalizi katika matumizi ya simu zao za mikononi kwa kuepuka matusi na kusajili laini ambayo taarifa zake si kweli.

Naye Mkuu Msaidizi wa Kitengo cha uhalifu wa kimtandao kutoka makao makuu ya jeshi la polisi, Joshua Mwangasa alisema tangu mwaka 2015 takwimu za makosa yamekuwa yakiongezeka na kupungua.

“Ukiangalia mwaka 2015 tulipokea makosa 5,172,  2016  (9,441),  2017 (7889) na mwaka 2018 tulipokea 8,708  hapo utaangalia yanapanda na kushuka lakini nasema tunakoelekea 2020 tunakwenda katika kiwango cha juu cha matumizi ya teknolojia ambacho kila mtu shughuli zake zitakuwa kwenye simu.

“Tukumbuke hata vitabu vitakatifu vimeandika siku za mwisho maarifa yataongezeka hivyo kuanzia mwaka 2020 watanzania wataanza kutumia kiwango cha 5GB, ni lazima sasa kama polisi na TCRA tukaanza kutoa elimu ya kuwalimisha namna ya kuepuka kuingia kwenye makosa ya jinai.

“Matokeo ya matumizi mabaya ya mtandao wa kijamii yamegawanyika sehemu tatu, kwa upande wa kijamiini  unaleta mmomonyoko wa maadili, upande wa siasa inaleta uvunjifu wa amani na kundi la mwisho ni lipo kwenye uchumi na athari zake ni kuharibu mfumo muhimu wa kitaifa,”alisema.









Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti