• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

MAGEUZI YA SERA YA ELIMU YATACHANGIA WINGI WA UJUZI NA VIJANA KUJIAJIRI-WAZIRI MKENDA

Posted on: July 5th, 2023

MAGEUZI YA SERA YA ELIMU YATACHANGIA WINGI WA UJUZI NA VIJANA KUJIAJIRI-WAZIRI MKENDA


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof.Adolph Mkenda amesema mageuzi yajayo ya Sera ya Elimu nchini yatakayojikita kumuongezea ujuzi zaidi kijana akiwa shuleni yatachangia vijana wengi kujiajiri kulingana na mazingira yanayomzunguka.

Waziri Mkenda amesema hayo Julai 05,2023 wakati wa majumuisho ya ziara yake ya siku moja Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza baada ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wizara yake vikiwemo vyuo vya ufundi Veta,amebainisha mafunzo ya Amali kama yanavyojulikana yataanza muda siyo mrefu mara baada ya Sera hiyo kupita kwenye hatua za mwisho mwisho.

"Sera hiyo mpya itamtaka mwanafunzi kuwa shuleni kwa miaka kumi tu atasoma hadi darasa la sita akifaulu atalazimika kuingia kidato cha kwanza hadi cha nne huko sasa atakutana na mafunzo kwa vitendo zaidi na akihitimu anatoka na ujuzi husika utakaokuwa mkombozi katika shughuli aliyolenga", amefafanua Prof Mkenda.

Kiongozi huyo mwandamizi wa Serikali ameongeza kuwa Mkoa kama wa Mwanza mafunzo hayo ya Amali yatawanuisha wale watakaojikita kwenye Uvuvi kwani wakihitimu watakuwa na ujuzi wa kutosha kwenye sekta hiyo tofauti na ilivyo sasa.

Waziri Mkenda amebainisha utekelezaji huo ni ahadi ya Rais Dkt.Samia Suluhu aliyoitoa Bungeni ya kuleta mageuzi kwenye sekta ya elimu kwa kutaka yawepo mafunzo zaidi ya kuwaongezea ujuzi ili kuweza kuzimudu fursa mbalimbali zilizowazunguka.

"Huu mchakato wa sera mpya ya elimu umeanza siku nyingi kwa kuwashirikisha wataalam na wadau,nawathibitshia sasa upo ukingoni kusubiri hatua kadhaa za mwisho mwisho za kupitiwa na Makatibu wakuu na Baraza la Mawaziri kabla ya kumfikishia rasmi Rais ili kumuomba aridhie,"Prof.Mkenda

Akiwa kijiji cha Karumo Wilayani Sengerema Waziri Mkenda ameshuhudia maandalizi ya ujenzi wa Chuo Kikuu Ardhi Kampasi ya Mwanza kitakacho kamilika Octoba mwakani kilichoghalimu zaidi ya Shs bilioni 18.

"Mhe Waziri Chuo hiki kitachukua muda wa miezi 15 kukamilika na kuanza kutoa mafunzo,wiki chache zijazo tunatarajia kumpata Mkandarasi,hapa kutakuwa na kozi 35 zikiwemo za kuwapata Wataalamu wa kupima ardhi kupitia majini, watatuzi wa migogoro ya ardhi na mafunzo ya amali pia yatatolewa hapa chuoni,"Prof.Evaristo Liwa,Makamu Mkuu Chuo Kikuu Ardhi.

Aidha Waziri Mkenda ameshauri mara baada ya Chuo hicho kukamilika kuwepo na mpango wa kuwapata baadhi ya wahadhili kutoka nje ya nchi watakaongeza utoaji wa elimu bora na kubadilishana uzoefu na watalaam wa hapa nyumbani.

Waziri huyo wa Elimu,Sayansi na Teknolojia akiambatana na Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mhe. Seni Ngaga amefika Halmashauri ya Buchosa na kushuhudia maandalizi ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi Veta kitakachoghalimu Shs bilioni 3.


Pia akiwa mjini Sengerema amekubali kukipokea Chuo cha Ufundi Veta mara baada ya uongozi kuwasilisha barua rasmi ya ombi hilo,  awali Chuo hicho kilikuwa kinamilikiwa na Halmashauri ya Sengerema.

"Mhe Waziri tumefarijika na ujio wako ambao kwa kweli umetutia shime na mpango ujao wa sera mpya ya elimu,tumejipanga vizuri kuongeza maeneo kwa ajili ya kuongeza madarasa yatakayo kidhi mpango huo wa Serikali ambao utakuwa ni muorobaini wa ukosefu

 wa ajira kwa vijana wetu,"Seni Ngaga,Mkuu wa Wilaya Sengerema.


Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti