Mama Anna Mkapa awasili Mwanza kuzindua Kitabu cha maisha ya Rais mstaafu awamu ya tatu, Hayati Benjamin Mkapa
Mama Anna Mkapa amewasili Mkoani Mwanza kwa ajili ya kushiririki Kongamano la Kitaaluma la Uzinduzi wa Kigoda cha Uprofesa pamoja na Uzinduzi wa Kitabu Cha Maisha ya Rais wa Awamu ya Tatu Hayati Benjamini William Mkapa litakalofanyika Jumamosi tarehe 12 Novemba, 2022 katika Chuo Kikuu cha Mt. Augustino cha Tanzania.




