• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Matukio yanayotokea yatambulisha Mwanza Kiuchumi - Mongella

Posted on: October 25th, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mhe. John Mongela amesema Serikali imeuweka mkoa huo kimkakati na uwekezaji kutokana na kuwa kitovu cha Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Akizungumza na waandishi wa habari  juu ya uwepo wa shughuli mbalimbali ndani ya mkoa huo kwa wiki moja mfululizo,Mhe. Mongella alisema ili  nchi ama mkoa  wowote uweze kujulikana  kimataifa ni lazima kuwepo na matukio yanayotambulisha kiuchumi,kijamii na kiutalii.

Alisema kuazia Oktoba 25 hadi Septemba Mosi, mwaka huu kutakuwa na shughuli ama matukio mbalimbali yakiwamo matamasha, warsha, mikutano ya  kitaifa na kimataifa ndani ya mkoa ambayo itasaidia kukuza uchumi na kuibua fursa na maendeleo ndani ya jamii.

Alisema Mwanza ni miongoni mwa mikoa michache  nchini ambayo  Serikali imeiweka kimkakati  wa  maendeleo na uwekezaji kutokana na kuwa kitovu cha EAC hivyo kufanyika shughuli mbalimbali mkoani humo zitasaidia  kukuza uchumi wa mkoa sambamba na jamii wakiwamo wafanyabiashara kufaidika.

“Leo tutaanza kuadhimisha siku ya fimbo nyeupe ambayo inawahusu watu wasioona ambapo wanawaomba wana Mwanza tuungane  pamoja kuona namna kutatua changamoto zinazowakabili na hata  kuthibiti vyanzo vinavyosababisha hali hiyo.

“Pia Oktoba 27 ,mwaka huu mkoa wa Mwanza utakuwa na tamasha la  Tigo fiesta na siku inayofuata tutakuwa na mashindano ya Rockycity Marathon ambayo yatahusisha mbio za kilomita kuanzia tano hadi 42 ambapo nchi mbalimbali zitashiriki.

“Vile vile Oktoba 29-30, mwaka huu kutakuwa na kongamamo la ndege zisizo na rubani ambapo shughuli hii itakuwa ya kimataifa, kama mnavyojua teknolojia imekuwa sasa  ndege hizo zitakuwa zinatumwa kwenda maeneo mengine na kutoa huduma kwa jamii, mbali na matukio hayo siku zinazofuata tutakuwa na shughuli ya  maadhimisho ya siku ya Mwalimu yatakayokwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 25 ya  Chama cha Walimu Tanzania (CWT) na kitaifa yatafanyika Mwanza,”alisema.

Mongela alisema faida za kijamii  na kiuchumi zitakazopatikana kwa matukio hayo ni kujenga ushirikiano ndani ya jamii, vijana kupata fursa za kuonyesha vipaji vyao, wafanyabiashara wa hoteli kupata wateja.

Hata hivyo aliongeza kuwa katika matukio hayo, Serikali mkoani humo imejipanga kutumia fursa hiyo kuwaelezea namna Mwanza ilivyo  na mazingira salama na rahisi kuzifikia hifadhi za taifa ikiwamo Serengeti.

Aliwataka wadau mbalimbali wanaohitaji uwekezaji ndani ya Mkoa wa Mwanza kujitokeza na kupewa ushirikiano na Serikali ili lengo la kimkakati liweze kutimia.



Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti