MKUU WA WILAYA YA ILEMELA AMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA MWANZA
Leo Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mhe. Amir Mohammed Mkalipa, amemtembelea ofisini kwake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa lengo la kujitambulisha na kusaini kitabu kufuatia uteuzi na uhamisho wa Viongozi alioufanya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 23 Juni, 2025 ambapo alimuhamisha Mhe. Mkalipa kutoka Wilaya ya Arumeru kuja Wilaya ya Ilemela.

Mhe. Mkalipa anachukua nafasi ya Mhe. Hassana Masala aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo.
