• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Mongella atoa ahadi mabati 100 ujenzi wa madarasa Kisiwa cha Kweru

Posted on: February 12th, 2020


Wananchi wa kisiwa cha Kweru mto ndogo kilichopo wilayani Ukerewe wamelazimika kujenga shule ya msingi ili kunusuru maisha ya watoto wao waliokuwa wakilazimika kuvuka maji kwenda ng’ambo ya pili kuifuata elimu kwa kutumia mitumbwi.

Akizungumza wakati wa ziara Mkuu wa wilaya hiyo Mhe.Cornel Magembe alisema Shule ya Msingi Shikizi ilijengwa kwa usimamizi wa polisi hiyo, ni baada ya kuibuka kundi la watu wakidai eneo hilo kuna makabuli ya babu zao lengo likiwa ni kukwamisha harakati za ujenzi wa shule hiyo.

Alisema kipindi cha nyuma watoto walilazimika kupanda mitubwi kuifuata elimu kisiwa jirani jambo ambalo lilisababisha watoto kupata adha mbalimbali hivyo wananchi waliungana na kuweza kujenga vyumba vinne vya madarasa,ofisi moja na matundu ya choo mawili.

“Shule hii ni mradi uliogharimu Tsh 33,000,000/- ambapo inahusisha mchango wa Mkurugenzi, Mchango wa wananchi pamoja, NMB  na mifuko 193 ya saruji fedha za Mfuko wa jimbo, katika kisiwa hicho”alisema Mhe.Magembe.

Awali mwenyekiti wa Halmashauri hiyo ambaye ni diwani kata ya Kanguli George Nyamaha amemweleza adhima ya wananchi wa kisiwa hiko kuwa ni kuboresha elimu na wapo tayari kukamilisha ujenzi kwa mifuko 193 iliyotolewa na Mbunge ili kupatiwa usajili hivyo wananchi wa kisiwa hicho walilazimika ujenzi wa shule kutokana na changamoto hiyo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella aliwapongeza kwa maendeleo hayo kwani kuna maeneo ambayo yanawakazi wengi lakini hawana hamasa ya kujenga shule hivyo alimuagiza Afisa Elimu wa Mkoa Michael Ligola kualakisha usajili wa shule hiyo ili kuwanusuru na adha hiyo, na kuahidi kuchangia bati mia moja ili kuunga mkono juhudi za wananchi hao.


“Kuna maeneo watu ni wengi na wanashindwa ata kujenga shule, ujenzi kwao ni ugomvi na mabishano wananchi wote wangekuwa kama wakazi wa kisiwa hiki tungekuwa mbali sana kimaendeleo na nitafuatilia madarasa mawili yaliyosalia pamoja na ujenzi wa Choo ili shule hiyo ipatiwe usajili kamili.”alisema  Mhe.Mongella.

Naye Afisa Elimu Mkoa Michael Ligola alisema Shule hiyo inatakiwa kusajiliwa ili kuwanusuru watoto hao hivyo wajitahidi kumalizia madarasa mawili na matundu ya vyoo ili kukudhi vigezo baada ya hapo watawapitisha wakaguzi na shule hiyo itasajiliwa.

Aidha wananchi wa eneo hilo wakizungumza katika mkutano wa hadhara Frank Vicent na Yusta John walisema baada ya watoto kushindwa kwenda shule unapovuma upepo ziwani wamechukua hatua hiyo ambapo hatua ya kwanza walianza na ujenzi wa shule kwa kutumia mabanzi ,wanafunzi walisoma hadi pale walipojenga shule hiyo  pia waliiomba serikali kusaidia kumaliza mapungufu yaliopo ikiwa pamoja na usajili wa shule hiyo.


Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti