• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Mradi wa Maji kisiwani Kome-Buchosa wa Shs Bilioni 2.2 kuanza Mei mwaka huu.

Posted on: March 1st, 2023


Zaidi ya wananchi Elfu 17 kati ya elfu 58 kwenye Vijiji 8 Kisiwani Kome - Buchosa wanatarajia kunufaika na Mradi mkubwa wa Maji unaotekelezwa na Kampuni Kamba's Company Group chini ya usimamizi wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini  (RUWASA) kwa zaidi ya Bilioni 2.2

Hayo yamebainishwa leo wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Malima wakati alipotembelea Mradi huo kwenye kijiji cha Lugata na kubaini kuwa Ujenzi wa Mradi huo uliofikia asilimia 70 ya ujenzi upo kwenye hatua za mwisho za utekelezaji na kwamba ifikapo  Mei mwaka huu utaanza kutoa Maji.

Mhe. Mkuu wa Mkoa amesema kwa kushirikiana na Wizara ya Maji atahakikisha Mkandarasi analipwa fedha zilizobaki kwa wakati na kufuatilia hatua za kupata msamaha wa kodi kwa mujibu wa mkataba wa mkandarasi huyo ili kuvitoa vifaa vilivyokwama bandarini mara moja.

Baadae Mkuu wa Mkoa alikagua maendeleo ya taaluma kwenye shule ya Sekondari ya Lugata na kusikitishwa na matokeo mabaya ya ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha nne pamoja na uwepo wa Miundombinu rafiki ya madarasa na akaagiza kukamilishwa kwa Ujenzi wa mabweni ili kuwapunguzia umbali wa kutembea wanafunzi wanapofika na kutoka shuleni hapo.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Lugata, Mbunge wa Jimbo la Buchosa Mhe. Erick Shigongo amesema ukamilishaji wa mradi huo utasaidia kuwaokoa akina mama wanaokamatwa na Mamba ziwani kwa kufuata Maji na kwamba suala la Magonjwa ya Tumbo kutokana na matumizi ya maji yasiyo salama itakua historia.

"Nimesikitishwa sana na maendeleo ya watoto kwenye shule hii, hatutafikia ndoto ya mafanikio kwa kufelisha watoto na ninatoa changamoto kwa walimu kutimiza wajibu na Serikali ihakikishe inatuletea walimu wa kutosha ili ujenzi wa madarasa uende sambamba ufaulu mzuri wa watoto." Amesema Mhe. Mbunge akiwa katika shule ya Sekondari ya Lugata.

Akizungumzia mradi wa Maji, Kaimu Meneja wa RUWASA Buchosa Mhandisi Elisha Sembo  amebainisha sababu za kuchelewa kwa mradi huo kwa Miezi 6 kuwa ni pamoja na kuchelewa kwa kuwasili kwa vifaa kutokana na taratibu za msamaha wa Kodi kwa vifaa vilivyonunuliwa nje ya nchi.

Naye, Ndugu Yahya Yusuph Mwenyekiti wa Kampuni ya Kamba's Company Group anesema kuwa endapo malipo ya fedha zilizobaki yatafanyika kwa wakati na kupatiwa msamaha wa kodi kwa vifaa vilivyopo bandarini mradi huo utakamilika kufikia  Mei 2023

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti