• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI MWANZA KUWA WABUNIFU UHABARISHAJI UMMA

Posted on: July 19th, 2024

MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI MWANZA KUWA WABUNIFU UHABARISHAJI UMMA


Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bwana Thobias Makoba amewataka Maafisa Habari wa Serikali Mkoani Mwanza kubuni habari mpya za kimkakati zenye kuitangaza miradi ya maendeleo ya Serikali badala ya kusubiri matukio.

Bwana Makoba ameyasema hayo leo Julai 19, 2024 wakati alipokua akizungumza na Maafisa Mawasiliano kutoka Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa, Taasisi, Mashirika na Makampuni  mbalimbali ya Serikali Mkoa wa Mwanza katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.

Bwana Makoba amesema anatamani kuona Maafisa hao wakiwa wabunifu zaidi katika kuhakikisha wanauhabarisha umma kwa namna ambayo siyo ya kutegemea habari kutoka kwa viongozi tu bali  watumie mbinu mbalimbali ili kuonesha utofauti wa utendaji wa sasa na siku za nyuma.

"Na hapa Mwanza ninajua kuna miradi mbalimbali ya kimkakati kama vile ujenzi wa reli ya SGR hivyo tusisubiri ijitokeze  dosari ukimbilie kutoa taarifa ya ufafanuzi , ni wakati sasa wa kubadili  namna ya utoaji wa taarifa zetu". Amesisitiza Makoba.

Aidha, amesema umekua ni utaratibu wake kukutana na Maafisa Mawasiliano kila mahali aendapo lengo likiwa ni kujitambulisha lakini pia kusikiliza na kuchukua maoni, mawazo na mapendekezo mbalimbali ambayo yatasaidia kuboresha utendaji kazi.

"Kuwa msemaji mkuu siyo kwamba unajua kila kitu, tunategemeana katika kuhabarisha kwani Serikali ni moja, " amefafanua Makoba.

Awali, Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bw. Balandya Elikana amesema Mkoa wa Mwanza ni Mkoa wa kimkakati kwa kuwa ndiyo lango kuu kwa kanda ya ziwa na ndiyo kitovu cha uchumi hivyo Maafisa Habari wanategemewa kwenye uhabarishaji na Serikali inawapa ushirikiano mzuri.

Naye Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali (RS Mwanza) Bw. Paulo Zahoro amesema hali ya uhabarishaji kwa Mkoa wa Mwanza ni nzuri hata kufikia hatua ya kushinda nafasi ya pili na kupata Kikombe na Cheti cha ushindi kutoka kwa Waziri wa Habari Mhe. Nape Nnauye kwenye Kongamano la Habari lililofanyika jijini Dar es Salaam Juni mwaka huu.

Maafisa Mawasiliano nao wamemshukuru Msemaji Mkuu wa Serikali kwa kutambua umuhimu wao ambapo wamemuahidi kutimiza wajibu wao kwa kuhabarisha jamii juu ya mambo mbalimbali yanayotekelezwa na Serikali.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti