• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

MTANDA ATETA NA WATUMISHI KWIMBA, ATAKA NIDHAMU KAZINI ILI KUWALETEA MAENDELEO WANANCHI

Posted on: June 6th, 2024

RC MTANDA ATETA NA WATUMISHI KWIMBA, ATAKA NIDHAMU KAZINI ILI KUWALETEA MAENDELEO WANANCHI


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo Juni 06, 2024 amezungumza na watumishi wa Halmashauri na Wilaya ya Kwimba Kwimba na akatumia wasaa huo kutoa dira ya kuwaletea wananchi maendeleo kupitia majikumu yao kuwa ni uzingatiaji wa nidhamu katika kazi.

Akizungumza na watumishi hao kwenye Ukumbi wa Halmashauri, Mtanda amewataka watumishi hao kuacha kuishi kwa mazoea na badala yake wawe na nidhamu ya kuwahi kazini na kujituma ili kuhakikisha wanawatumikia wananchi kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za miongozo.

Aidha, amewataka amewataka watumishi kujenga umoja baina ya taasisi moja na ingine ndani ya wilaya na kushirikiana kwenye kazi na kuepuka tabia ya ubishani au makundi kazini ili kila mmoja ajue ana wajibu wa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria na sio kwa ajili ya mtu fulani na vinginevyo.

Vilevile, amewapongeza kwa ukusanyaji wa Mapato hadi kufikisha shilingi Bilioni 3.5 kutoka Bilioni 2 za siku za nyuma na amewakumbusha kutumia fedha kwa mujibu wa Miongozo iliyopo kwa kutenga 10% za Makundi ya kisheria, 40% za miradi ya maendeleo na kuhakikisha wanaweka fedha benki.

Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija amesema kuwa upatikanaji wa Maji vijijini kwa sasa ni asilimia 62 na ipo miradi kadhaa ya maji inaendelea kutekelezwa na kwamba itakapokamilika itasaidia wilaya hiyo kufikia asilimia zaidi ya 70 ya upatikanaji maji safi.

Aidha, amebainisha uwepo wa nishati ya umeme kwenye vijiji vyote wilayani huku akifafanua kuwa ukusanyaji wa mapato kupitia TRA wamekusanya zaidi ya Bilioni 2 tofauti na Bilioni 1 waliyoikusanya mwaka uliopita ikiwa ni ongezeko linalotokana na sera nzuri za serikali ya awamu ya sita.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti