• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Mwanza Kutokomeza vifo vya mama,watoto wachanga

Posted on: April 3rd, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongella amewasainisha  kiapo  cha uwajibikaji wakuu wa wilaya zote za Mkoa huo  juu ya kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wachanga ambapo amewataka kila mmoja awajibike katika eneo lake na  kutoa taarifa ya za utekelezaji.

Mhe.Mongella alisema kutokana na jitihada za Serikali za kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga, mwaka 2018 vifo hivyo vimepungua na kufikia 151 lakini kuanzia Januari mwaka huu tayari vifo 46 vitokanavyo na uzazi vimetokea ndani ya mkoa huo.

“Sababu zinazoelezwa kusababisha vifo hivyo ni kwamba shinikizo la damu, kifafa cha mimba, kuvuja damu nyingi lakini sababu zingine inadaiwa zinatokana na maamuzi katika familia husika, vile vile na sisi viongozi wa umma tunahusika katika maeneo fulani.

“Sasa mimi    kama Mkuu wa Mkoa naamua niingia mikataba na wakuu wa wilaya zote za mkoa huu, mkataba huu pia utawahusu wakurugenzi,meya na wenyeviti wa halmashauri, viongozi hawa  niliowataja itakuwa rahisi mimi kuwabana na ndio maana nataka waje hapa mbele waweke sahihi zao.

“Kila mmoja akitoka hapa aende awajibike katika eneo lake kwa kufuatilia maendeleo ya utoaji huduma katika vituo, zahanati na hospitali zao, pia ni muhimu wakashuke  ngazi za chini kuanzia vitongoji hadi vijiji na kuwatambua wajawazito na  maendeleo yao, ikitokea kifo  katika eneo lako unapaswa kutoa  sababu za msingi kilichosababisha,”alisema Mongella.


Mongella alisema kumekuwapo na tabia ya viongozi  wengi wa Serikali kuzungumza wakiwa maofisini  kitendo ambacho kimeshindwa kuwa na mafanikio chanja kwa jamii  juu ya mikakati inayopangwa, hivyo ni wakati muafaka kwenda vijijini na kuzungumza moja kwa moja na wananchi.


Alisema licha ya Serikali kuboresha sekta ya afya kwa kujenga vituo vya afya, zahanati, hospitali sambamba na kuongeza bajeti lakini tunapaswa kujitafakari kinachosababisha vifo vya mama na watoto vinaendeleo kutokea, hivyo aliwataka wadau wote wa afya, vyombo vya habari, viongozi wa dini na waganga wa tiba asili kuungana na kuelimisha jamii kuwahi kwenye tiba sahihi.

Naye Mratibu wa Afya mama na mtoto Mkoa wa Mwanza, Cecilia Mrema  kuna haja ya Serikali kuboresha magari ya kubebea wagonjwa mkoani humo kwani kati ya ambulesi 9 kati 25 zilizopo ndizo zilizo na vifaa vyote vya kutolea huduma wakati mgonjwa akipelekwa hospitali ya rufaa.


Alisema katika Mkoa wa Mwanza sababu nyingi za vifo hivyo ni  upungufu wa damu, vifaa, baadhi ya watumishi wa sekta ya afya kutokuwa na uelewa zaidi kwa wagonjwa wanaohitaji msaada wa haraka, gari za wagonjwa kutokuwa na mafuta na vifaa vyote vya tiba.

Vile vile alisema wajawazito kutumia dawa za kienyeji, kifafa cha mimba ambapo aliwataka akinamama kuhudhuria katika vituo vya afya  ili kupata tiba sahihi.

Kwa upande wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dkt. Thomas Rutachunzibwa alisema  uzinduzi wa kampeni ya uwajibikaji katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi yenye kauli mbiu ya ‘Jiongeze Tuwavushe salama’  ni utekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu alilolitoa Novemba mwaka jana kwa kuelekeza kila mkoa kuweka mikakati ya kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Alisema   kutokana na agizo hilo, mkoa wa Mwanza  umejipanga kupitia kampeni hiyo kupunguza idadi ya vifo vya mama na mtoto ambapo aliwataka watoa huduma kuongeza kasi kwani Serikali imeelekeza nguvu kubwa katika sekta ya afya.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti