• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Mwanza waaswa kujitokeza kujiandikisha katika orodha ya mpiga kura

Posted on: October 8th, 2019

Zoezi la uandikishaji wananchi kwenye daftari la Mkazi mkoani Mwanza kwa ajili ya kurasimisha orodha kamili ya wapiga kura watakaoshiriki uchaguzi wa serikali za mitaa limeanza rasmi tarehe 8 ambapo litadumu hadi Octoba 14.

Akizungumuzia hali hiyo Msimamizi msaidizi wa kituo cha uandikishaji cha Polisi eneo la wazi mtaa wa PPF kata ya Kiseke Hellen Mcharo amesema mara nyingi watu husubiri siku zibaki chake ndiyo wajitokeze.

"Tumefungua kituo kwa wakati naona wananchi wanajitokeza wachache wachache  mara nyingi huwa wanasubiri hadi siku zipungue,"alisema  Mcharo.

"Kwa sababu ndiyo siku ya kwanza tunaamini kutokana na hamasa inayoendelea kutolewa basi kuanzia kesho idadi itakuwa kubwa zaidi ya leo."

"Sisi kama waandikishaji na wasimamizi  tunaendelea kuwahimiza viongozi wa vyama na serikali kutoa hamasa ili kuongeza  mwitikio wa wananchi kwenye zoez hili ili likamilike kwa wakati.

"Pia tunawaomba wale wananchi wachache waliojitokeza wawe kama mabalozi kwa wengine,  nawaishi  nao, wakazi wa Mwanza waachane na utamaduni wa kusubiri dakika za mwisho kwani tukumbuke zeozi hili ni la muda mfupi hivyo wajitokeze  mapema na kwa wingi ili tumalize kujiandikisha tuanze kujiandaa na uchaguzi,"alisema Mcharo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza  Mhe. John Mongella, amesema kuwa ili kuongeza mwamuko kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha hamasa ya matangazo inatakiwa kufanywa usiku na mchana kila mtaa ili ambaye hajapata taarifa mchana basi aipate usiku.

"Mpaka sasa zoezi bado naliona linaenda taratibu japo ndiyo tunaanza niwasihi viongozi wa vyama ma serikali tushirikiane kuongeza  hamasa na wanaohusika  kufanya matangazo basi wafanye hivyo hasa wakati wa usiku ili ambao hawana taarifa hizi wazipate kwa utulivu zaidi, alisema Mongella.

"Nazani hata wasimamizi mnaona  wenyewe hadi sasa mmeshaandikisha wananchi ambao ni wachache sana ikilinganisha na idadi halisi ya wakazi wa mtaa huu  wanaotambulika mtaani kwenu kitu ambacho kinatukumbusha kuwaamusha zaidi wasio na taarifa.

"Tuhimizane usiku kucha ili tufanikishe zoezi hili kwa maaana wapo wengine bado uelewa wao ni mpaka wapate msisitizo ndiyo wanaelewa hivyo tujitahidi twende wote tuhakikishe hakuna mwananchi anayebaki nyuma ili mwisho wa siku uchaguzi utakapofika wananchi washiriki kwa wingi," alisema Mongella.

Mmoja ya wakazi  wa mtaa wa Buswelu A aliyejitambulisha kwa jina la Denis Jackson baada ya kujiandikisha ametoa wito kwa wananchi wengine kuja kwa wingi kujiandikisha kwani mbali na kuwa kufanya hivyo kunatoa haki ya msingi ya kupiga kura lakini pia zoezi la uandikishaji linakamilika ndani ya muda mfupi na halina usumbufu. 

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti