• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Mwanza Yaadhimisha fimbo nyeupe kitaifa

Posted on: October 23rd, 2018


Chama cha wasioona Tanzania (TLB) kimesema kuwa hakina tatizo na uongozi wa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Magufuli kutokana na changamoto zilizokuwa zinazokikabili chama hicho kupungua siku hadi siku.

Kauli hiyo imetolewa  jijini hapa na Mwenyekiti wa Chama cha Wasiona Tanzania Mkoa wa Mwanza Musa Mashauri  juu ya maandalizi ya maadhimisho ya fimbo nyeupe ambayo kitaifa yanafanyika mkoani Mwanza.


Mashauri  amesema TLB inamshukuru Rais John Magufuli kwa upendo wa dhati kwa watu wenye ulemavu wa kutoona na walemavu wengine  nchini kwa kuwathamini na kufanya maamuzi stahiki ya kumteua mmoja wa walemavu Amon Mpanju kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

“Niseme tu sisi tunamshukuru sana Rais wetu mpendwa, anatujali na anatuthamini, nasema na mwandishi kaandike hivyo kwamba sisi hatuna shida na rais wetu kwa sasa tunampenda kwa jinsi anavyotujali,”alisema.

Akizungumzia maandalizi ya maadhimisho hayo yatakayoadhimishwa kwa kauli mbiu, “ Mafunzo ya Tehama kwa wasioona ni nyenzo jumuishi katika uchumi wa viwanda,” alisema maandalizi muhimu yamekamilika.

Alisema uamuzi wa maadhimisho hayo kitaifa kufanyika mkoani Mwanza ulifikiwa baada ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya TLB kwenye kikao chake kilichofanyika mjini Morogoro kuja na uamuzi huo.

Alisema tangu wakati huo shughuli mbalimbali za maandalizi zimekuwa zikifanyika kwa ajili ya kufanyika maadhimisho hayo, ambayo yanafanyika katika Viwanja vya Furahisha  ambayo kilele chake ni Oktoba 25 mwaka huu.

“ Mfano tuliwasilisha barua kwa Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella kuomba mkoa wake kuwa mwenyeji wa maadhimisho haya kitaifa na alilikubali ombi letu,” alisema.

Alisema kwa msaada wa Mongella, imeundwa kamati maalum ya mkoa ya watu 20 ambayo imepewa jukumu la kuratibu maadhimisho hayo ambayo inaongozwa na Katibu Tawala Msaidizi (Miundombinu) Seif Hussein.

“ Kamati hiyo imetengeneza mpango kazi wa bajeti kwa ajili ya maadhimisho hayo, ambapo jumla ya Sh. milioni 74 zinahitajika, lakini kutokana na michango ya vifaa kwa ajili ya watu wasioona, naweza kusema tumepata karibu asilimia 80 ya lengo ”, alisema.

Aliwashukuru watu waliosaidia kufanikisha michango  hiyo ikiwemo serikali ya mkoa wa Mwanza, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na Mkurugenzi wa the Desk and Chair Foundation Sibtain  Meghjee na wadau wengine wanaoshirikiana nao Mobiles Eyes Foundation Tanzania, Beta Charitable Trust, Flora  na Bilal Muslim Tanzania ambao kwa pamoja wamechangia vifaa mbalimbali vya tiba, zikiwemo fimbo nyeupe, miwani na vifaa vya upasuaji vyenye thamani ya Sh milioni 20.

“ Lakini pia kupitia maadhimisho haya, tumefanikiwa kuandaa siku ya macho, ambapo wananchi wenye matatizo ya macho watapata huduma bure ya upimaji wa macho na tumeandaa maonesho ya wajasiriamali kwa wasioona lengo likiwa ni kuionyesha jamii kuwa wasioona sio ombaomba na wao wanaweza kufanya kazi na kujipatia kipato,” alifafanua.

Alisema kutokana na ufinyu huo wa bajeti, baadhi ya shughuli ambazo zilipangwa kufanyika kwenye maadhimisho hayo zimeondolewa. Alizitaja shughuli hizo zilizoondolewa kuwa ni upandaji wa miti 400 kwa ofisi za wakuu wa wilaya za Nyamagana na Ilemela, Shule Maalum ya wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi ya Mtindo iliyoko wilayani Misungwi.


Akikabidhi vifaa hivyo kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dkt. Philis Nyimbi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mkurugenzi wa the Desk and Chair Foundation Sibtain Meghjee alisema wametoa vifaa hivyo kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali za kuwasaidia watu wenye ulemavu nchini.  

Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dkt.Philis Nyimbi aliishukuru taasisi ya the Desk and Chair Foundation kwa moyo wako wa upendo wa kuwajali watu wenye ulemavu na mahitaji yao na kuyaomba mashirika na wadau wengine wa maendeleo kuiga mfano wao.

Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa (RMO) Dkt.Silas Wambura akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo, alithibitisha kuwa vifaa hivyo vinafaa kwa huduma za utoaji wa tiba na kinga kwa jamii ya watu wasiiona nchini.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi hayo Seif Hussein alisema maandalizi kwa ajili ya maadhimisho hayo yamekamilika na kwamba Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia ulemavu Mhe.Stela Ikupa.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti