• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Mwanza Yaweka mikakati madhubuti katika kuimarisha Sekta ya Afya

Posted on: February 4th, 2020

Mkoa wa Mwanza umetangaza rasmi mkakati madhubuti  maeneo yote ya vivuko,bandari pamoja na uwanja wa ndege wa kimataifa  wa jijini Mwanza,kwa wageni wote wanaoingia mkoani humo  kutoka nje ya nchi kufanyiwa vipimo ili kubaini kama wameathirika na homa ya mafua makali yanayosababishwa na kirusi aina ya corona.

Afisa Afya Mkoa wa Mwanza Fungo Masalu akizungumza wakati wa  kujadili masuala ya lishe,afya ya uzazi hususani kwa mama mjamzito,mtoto pamoja na tahadhari ya magonjwa ya homa ya manjano na homa ya mafua makali yanayosababishwa na kirusi kipya aina ya corona yanayoendelea katika nchi mbalimbali alisema, mkakati uliopo ni kuimarisha mipaka ambayo inaingiza wageni.

“Tumeweka utaratibu wa kupima joto la mwili endapo mtu akiwa na joto homa kali atafanyiwa uchunguzi kubaini alipotokea yawezakuwa ametokea nchi iliyoathirika kwa sababu hali yake imeashiria kuwa na ugonjwa”alisema Masalu.

Aliongeza kuwa elimu ya afya itatolewa kwa umma hususani kipindi hiki kabla ya ugonjwa kufika nchini ili waweze kuzingatia kanuni za afya katika kujikinga na ugonjwa huo.

Awali ya yote Mratibu wa huduma ya mama na mtoto Mkoa wa Mwanza Cecilia Mrema,akitoa taarifa ya huduma ya afya ya uzazi na mtoto na hali ya vifo vya wazazi alisema, kwa mwaka jana mama wajawazito waliopoteza maisha kwa kutokwa na damu nyingi pamoja na kifafa cha mimba wakati wa kujifungua walifikia asilimia 40, hivyo wameweka mkakati ili kumaliza tatizo hilo ambapo hatua ya kwanza ni kuhakikisha upatikanaji wa damu unakuwa wa uhakika wakati wote.

Pia aliwataka wajawazito wote kupima wingi wa damu mapema ili ikibainika anakiwango kidogo cha damu waweze kumsaidia mapema akiwa kwenye huduma za wajawazito kabla ya wakati wake wa kujifungua endapo akichelewa hatutaweza kumsaidia katika hatua ya mwisho.

Akifungua kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Dkt.Emmanuel Kipole kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella,alisema umasikini wa kipato,machafuko ya kisiasa  na sera zisizo tambua umuhimu wa lishe ndio chanzo kikubwa cha jamii kuwa na lishe duni.

Pia uelewa huo mdogo wa masuala ya lishe umechangia suala hilo kutokupewa kipaumbele katika mipango na bajeti hususani katika ngazi za halmashauri ambapo ndipo walipo watoto, vijana na wanawake wanaohitaji huduma bora za lishe .

“Serikali kwa kutambua lishe ni suala la kimaendeleo hapa Tanzania mapambano dhidi ya lishe duni yamekuwa ni moja wapo ya maeneo yaliyopewa kipaumbele katika mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano ulianza mwaka 2016-2017 na 2020-2021,”alisema Kipole.



Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti