• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Mwanza Yatoa Tahadhali ya ugonjwa wa Ebola

Posted on: May 17th, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella amewataka Maofisa afya, waganga wakuu wa wilaya, kamati ya ulinzi na usalama,viongozi wa bandari na viwanja vya ndege kuhakikisha wanajikita katika kudhibiti ugonjwa wa ebola.

Mhe. Mongella ameyasema hayo wakati wa kikao cha kamati ya huduma ya afya ya msingi ya kuhakikisha kuwa ugonjwa huo hauingii nchini  hasa Mwanza  kwa kuwa ni Mkoa ambao ni kitovu kikubwa cha biashara hivyo kuna muingiliano mkubwa wa watu kutoka nchi nyingine.

Mhe.Mongella ameagiza kuweka vifaa tiba maalumu katika vituovya afya na maeneo yenye msongamano  wa watu,pia vifaa hivyo vitawanywe ili kuweka tahadhali ya kuepuka ugonjwa wa ebola ambao ni hatari kwa sasa kwa kuwa tayari umeishaingia Nchi jirani.    

 " RMO vifaa tulivyo navyo visikae kwenye hospitali ya Mkoa tu bali visambazwe kwenye vituo vilivyopo maeneo hatarishi kama Nyegezi, Buzuruga,soko la Butimba  na maeneo mengine yenye watu wengi hapa tupo kuchukua hatua za kujikinga" alisema Mongella.

Naye Mratibu wa chanjo Mkoa wa Mwanza Amos Kiteleja alisema umakini unahitajika ili kutambua dalili zake ambazo baadhi ni homa za mara kwa mara, kutoka damu sehemu zote za mwili zilizo wazi (matundu) ikiwa upatikanaji wake waweza kuwa kwa kugusana, mate, damu, kinyesi na majimaji kutoka kwa mgonjwa, kujamiana na watu tofauti .

Akielezea changamoto zinazowakabili ni kutokuwa na kituo cha Kuhudumia wagonjwa wa milipuko ukiwemo wa ebola, ukosefu wa vifaa vya kujikinga wakati wa kutoa huduma, mwingiliano wa watu kutoka maeneo mbalimbali hasa soko la mwaroni pamoja na uelewa mdogo kwa jamii juu ya ebola, pamoja na  mila na desturi.

Kiteleja aliongeza kuwa  mpaka sasa maeneo ambayo ni hatari ni soko la mwaroni kirumba, uwanja wa ndege wa Mwanza, bandari, vituo vya mabasi ya abiria,ukerewe na visiwa vyote, nyumba za kulala wageni, waganga wa jadi, nyumba za ibada na maombezi pamoja na vituo vya kutolea huduma za afya.

Jumhuri ya kidemkrasia ya Congo (DRC) ndio ugonjwa ulipo kwa sasa na tayari wagonjwa 34 wamepatikana na vifo 18 ikiwa ni Sawa na asilimia 52.9 baada ya kuripotiwa kuwepo kwa ugonjwa huo mei 11 mwaka huu ukiwa ni mlipuko wa tisa katika miongo minne iliyopita.


Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti