• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Mwanza yazindua Chanjo ya Mlango wa Kizazi na Polio

Posted on: April 23rd, 2018


Jumla ya wasichana 31291 Mkoani hapa wenye umri wa miaka 14, wanatarajia kupatiwa chanjo ya kuzuia saratani ya shingo ya kizazi.Chanjo hiyo itahusisha mabinti kutoka katika wilaya zote za Mkoa wa Mwanza walioko shuleni 26,641 na walio nje ya shule 4,650.

Akizungumza na wananchi pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mkuyuni C waliofika hospitali ya Nyamagana  kwa ajili ya kupata Chanjo hiyo, Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza Dkt. Silas Wambura alisema uzinduzi wa chanjo hii umefanyika leo april 23 katika hospitali ya wilaya ya Nyamagana Butimba ila chanjo itaendelea kwa vituo vyote na itakuwa ni bure.

 “Chanjo hii itaenda sambamba na maadhimisho ya wiki ya chanjo kitaifa ambayo yameanza leo April 23 hadi 30, pia chanjo hii imelenga mabinti kuanzia umri wa miaka 9 hadi 14 kwa ajili ya kuwakinga na saratani ya shingo ya kizazi ambayo imekuwa ni tatizo kwa wanawake nchini na duniani kote,” alisema Dkt.Wambura.

Pia aliongeza kuwa, kutokana na serikali kutokuwa na uwezo wa kugharamia chanjo hizo kwa sasa imeamua kuanza na mabinti wenye umri wa miaka 14 ila kadri wanavyo endelea wataanza kutoa kwa mabinti wenye miaka 9 hadi 13, na ndoto yao hapo baadae Nchi iweze kutengeneza chanjo hizo na dawa kama ilivyo dhamira ya Rais wa Jamuhuri ya Muungangano wa  Tanzania ya kuifanya  kuwa  ni nchi ya viwanda.

 Aidha,Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. alisema, mbali na chanjo hiyo pia kutakuwa na chanjo ya polio kwa njia ya sindano kwani mwanzo ilikuwa ya matone hivyo aliwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kwani chanjo hiyo ni salama na haina madhara kwa binadamu na imethibitishwa na Shirika la Afya Duniani(WHO) na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA).


Kwa upande wake Mratibu wa Chanjo Mkoa wa Mwanza Amos Kiteleja alisema, saratani ya shingo ya kizazi ina athari kubwa kwa afya ya wanawake ulimwenguni kote na inakadiriwa kila mwaka wanawake 466,000 wanathibitika kuwa na ugonjwa huo na wengi wao wako katika nchi zinazoendelea Tanzania ikiwemo.

Kiteleja alisema, ugonjwa huo unashika nafasi ya pili kwa kusababisha saratani kwa wanawake huku ya kwanza ikiwa ni ya matiti lakini ndio inayoongoza kwa kusababisha vifo nchini ambapo kwa ujumla wa zote mbili husababisha vifo vyote vya kinamama kwa asilimia 50 vitokanavyo na saratani.

“Saratani ya shingo ya kizazi husababishwa na virusi vya Papiloma (Human Papiloma Virus- HPV),huambukizwa kwa njia ya kujamiana katika umri mdogo,kuwa na wapenzi wengi,kuzaa watoto wengi na uvutaji wa sigara,” alisema Kiteleja.

Pia alisema, chanjo hiyo kwa mwaka huu itatolewa kwa wasichana wenye umri wa miaka 14 na baadaye itatolewa kwa Wote wenye umri wa miaka 9 hadi 14 kabla ya kutolewa kwa miaka 9 pekee hawana budi kupata wakiwa na umri mdogo kabla hawajaambukizwa HPV kwani ni kinga na siyo tiba.

Vilevile alisema, chanjo hiyo itatolewa kwenye vituo vyote vinavyotoa huduma za afya ya mama na mtoto zikiwemo hospitali,vituo vya afya, zahanati na sehemu zinapotolewa huduma tembezi na huduma za mkoba hususani shuleni na bila malipo kwa wenye umri wa miaka 14 na itakuwa inatolewa kila siku baada ya hii leo kuzinduliwa.

Aidha alisema, ili kupata kinga kamili wanatakiwa wapate chanjo mara mbili, hivyo dozi ya pili inatakiwa wapatiwe baada ya miezi sita, jamii inapaswa kuelimishwa na kuhamasishwa umuhimu wa chanjo hiyo na kujitokeza kwa wingi ili kumaliza tatizo hilo kwa kina mama.

Na kuongeza kuwa kwa wenye umri wa miaka 15 na kuendelea wanaweza kupata chanjo hiyo katika hospitali binafsi ambapo watachangia gharama na njia ya kujikinga ni kutembelea vituo vya kutolea huduma za afya ya mama na mtoto mara kwa mara ili kufanyiwa uchunguzi wa kina na wataalam na ikibainika dalili za mwanzo kupatiwa matibabu stahiki.

Naye Afisa Chanjo wa Clinton Health Access Initiative Joan Mungereza alisema, chanjo hiyo ina gharama kubwa serikali kwa sasa kutokuwa na uwezo wa kuwapatia wote wenye umri wa miaka 9 hadi 14 kwani kupitia Wizara ya Afya kwenye Mpango wa Taifa wa Chanjo una chanjo nyingi na zote zinatolewa bure hivyo mkakati na utoaji wa chanjo ni endelevu nchini katika kumaliza tatizo hilo kwa kina mama.

 

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti