• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Mwanza Yazindua soko la Madini

Posted on: May 8th, 2019



Waziri wa Madini, Doto Biteko amesema, katika kuhakikisha kwamba mchango wa sekta ya madini unaifikisha nchi kwenye uchumi wa kati ifikapo 2025, masoko ya madini ni muhimu.

Ameyasema hayo leo, alipokuwa akizindua soko la madini la Mkoa wa Mwanza ambapo amewataka viongozi mbalimbali wa serikali katika ngazi zote kushiriki kikamilifu katika kutekeleza mipango iliyowekwa na Serikali kupitia Wizara yake ili kuifikisha nchi katika uchumi huo wa kati.

Biteko amesema, wizara imechukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kikao cha Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu

Tawala wa Mikoa kilichofanyika mwezi Januari, 2019 Jijini Dodoma kikao kilicholenga kujenga uelewa wa pamoja juu ya maudhui ya kanuni wa uanzishwaji masoko ya madini nchini.


Aliendelea kusema, katika kuelekea uanzishwaji wa masoko ya madini nchini ulioanza mapema mwezi Februari, wizara ilifanikiwa kufanya mafunzo kwa Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi pamoja na Makatibu Tawala wa Wilaya.

Pamoja na jitihada hizo, Wizara ilifanikiwa kufanya Mkutano Mkubwa wa kisekta mwishoni mwa mwezi Januari 2019 na kupokea  maoni mbalimbali ya wadau yaliyopelekea Serikali kufanya mabadiliko ya sheria ya mwaka 2019 iliyohusisha utungwaji wa kanuni za masoko kwa ajili ya kuanzishwa masoko ya madini.


Aidha, Biteko amesema serikali ilikubali ombi la wadau la kupunguza utitiri wa kodi na tozo mbalimbali kwa wachimbaji wadogo na kuamua kufuta baadhi ya kodi hizo ikiwemo kodi ya zuio (withholding tax) pamoja na kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwa wachimbaji wadogo.

Akizungumzia historia ya uanzishwaji wa soko la madini mkoani Mwanza, Biteko alisema ilianza mnamo mwaka 2018 wakati wizara ilipounda kamati maalum kwa lengo la kubaini sababu ya utoroshwaji wa madini hasa madini ya dhahabu na vito.


Biteko anasema pamoja na hilo kamati ilibaini kuwa utitiri wa kodi na tozo mbalimbali zilizokuwa zikitozwa kwa wachimbaji wadogo wa madini ni sababu nyingine iliyochangia utoroshwaji wa madini nchini na kukiri chimbuko la uanzishwaji wa masoko ya madini kuwa ni Mwanza kupitia kamati hiyo.


“Uzinduzi wa soko hili unatoa majibu kwa maswali ya wananchikuhusu changamoto ya utoroshwaji wa rasilimali madini ambayo imedumu kwa muda mrefu” Biteko alikazia.


Aidha, Biteko amewataka wadau wote katika mnyororo mzima wa uendeshaji wa masoko ya madini kutimiza wajibu wao kwa uzalendo wa kiwango kinachostahili.


Kwa upande wake katibu Mkuu wa Madini, Prof. Simon Msanjila amewataka viongozi wa serikali kushiriki kikamilifu katika kusimamia rasilimali madini inayopatikana nchini.

Akielezea idadi ya masoko yaliyofunguliwa mpaka sasa, Prof. Msanjila alisema ni masoko ya madini 13 na siku ya leo masoko ya madini manne yanafunguliwa likiwemo la Mwanza, Kagera, Iringa na Songwe wakati taratibu za kukamilisha zoezi hilo kwa mikoa iliyosalia nchi nzima zikiendelea.


Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella alisema, Mkoa wa Mwanza unazalisha madini ya dhahabu na madini ya ujenzi kwa kiasi kikubwa katika wilaya ya Kwimba na Misungwi na kiasi kidogo katika maeneo ya Sengerema. Alikiri uwepo wa uzalishaji wa madini ya almasi kwa kiwango kidogo katika maeneo ya Mabuki na Manangwa wilayani Misungwi.

Mongella amebainisha kuwa wananchi wa Mkoa wa Mwanza wana imani kuwa usimamizi mzuri wa sekta ya madini utaipelekea nchi kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti