• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

NAIBU WAZIRI KATAMBI AONYA WANAOVAMIA SHAMBA LA MIFUGO MABUKI

Posted on: August 25th, 2023

NAIBU WAZIRI KATAMBI AONYA WANAOVAMIA SHAMBA LA MIFUGO MABUKI


Mhe. Patrobas Katambi, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) amewataka wananchi wanaoishi karibu na Shamba la Mifugo la Mabuki wilayani Misungwi hususani jamii ya wafugaji kutovamia eneo hilo lililotengwa na Serikali kwa ajili ya utafiti na ufugaji wa kisasa.

Ametoa agizo hilo leo Agosti 25, 2023 alipotembelea Shamba hilo na kuzungumza na Vijana 90 walio kwenye programu maalumu ya kuwajengea uwezo kiuchumi ambapo wananenepesha ng'ombe zaidi ya 900 kupitia vituo atamizi chini ya ufadhili wa Serikali.

Katambi amesema Serikali ya awamu ya Sita imeamua kurejesha hadhi ya shamba hilo lililoanzishwa na Rais Nyerere 1967 kwa kuwaletea vitendea kazi kama Matrekta mawili, Ng'ombe jike wa kisasa 500 pamoja na zaidi ya Milioni 650 kufadhili mradi huo nje ya mtaji na fedha za kujikimu wanazopewa vijana.

"Eneo hili ni lazima liheshimiwe kwani Serikali inawekeza kwa ajili ya maendeleo  ya wananchi wenyewe, naomba uongozi wa Shamba na Wilaya kwa ujumla tuendelee kuwaelimisha jamii inayozunguka shamba hili juu ya athari za uvamizi wao kwa maendeleo ya shamba hili." Amesisitiza.

Aidha, amebainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia imedhamiria kuwainua vijana kiuchumi na ndio maana imefanya maboresho kwenye Sera ya uchumi kwa vijana na kwamba siku za usoni itaanzishwa benki ya Vijana ambayo itawakopesha kwa dhamana ya maarifa yao.

Vilevile, ametoa wito kwa uongozi wa shamba hilo kutangaza soko la ng'ombe hao ili wauzwe na kununuliwa wengine na kunenepeshwa ili kukuza mitaji ya vijana hao waliotoka kwenye vyuo mbalimbali  nchini na kuwezeshwa mitaji chini ya mpango wa Ujenzi wa Kesho bora (BBT) sekta ya mifugo.


Naye, Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Ndugu Emily Kasagara aliyemwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa ametumia wasaa huo kuishukuru Serikali kwa mradi huo na akaahidi kuwa serikali ya Mkoa itashirikiana na uongozi wa shamba hilo katika kudhibiti ufugaji haramu unaofanywa na baadhi ya wananchi.

Bi Lini Mwala, Meneja wa shamba hilo amefafanua kuwa uwepo wa shamba hilo lenye zaidi ya hekari elfu 25 umesaidia wananchi kupata elimu ya ufugaji na mbegu bora na kwamba kuna jumla ya ng'ombe 2742, mbuzi 356 na nyati maji 59 huku zaidi ya 50 wakiwa wameuzwa kwa wananchi kwa ajili ya kusambaza mbegu hiyo.

Meneja wa chuo cha mafunzo ya uvuvi Jacob Ngowi amesema kuwa tangia kuanzishwa kwa kituo hicho cha Uatamizi zaidi ya ng'ombe 165 wameuzwa na kwa wastani kila mmoja anakua na ongezeko la Kilogramu hadi 45 baada ya kunenepeshwa na ameishukuru Serikali kwa ujenzi wa Miundombinu.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti