• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

NEMC yashauriwa kuziongezea meno baadhi ya Sheria zake za kulinda Mazingira.

Posted on: May 5th, 2023


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Adam Malima amelishauri Baraza la Taifa la Hifadhi ya usimamizi wa Mazingira Tanzania,NEMC kupitia upya baadhi ya Sheria zake za utunzaji wa Mazingira hasa za Kelele sumbufu ambazo zimekuwa kero kwa wananchi siku hadi siku.

Akizungumza kwenye kikao kazi cha Baraza hilo kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa uliokuwa unajadili uwepo wa matumizi ya mifuko ya Plastiki na Kelele sumbufu,Mhe.Malima amesema utoaji wa vibali kwa kumbi za starehe na nyumba za ibada usiozingatia Sheria na taratibu umechangia kusababisha kero kwa wananchi na ushahidi ni ofisi yake inayopokea malalamiko hayo kila uchao.

"Kelele sumbufu kwa kweli zinawatesa sana wananchi,kaeni pitieni vizuri Sheria zenu na ikibidi mkaziongezee adhabu zaidi,baadhi ya nyumba za ibada zinakiuka kabisa taratibu kwa kupaza sauti usiku kucha bila kujali athari zake kwa walio jirani,hii kwa kweli haikubaliki",amesisitiza Mkuu huyo wa Mkoa.

Kuhusu mifuko ya Plastiki Mhe.Malima ameishauri NEMC kuona namna ya kuwajali wafanyabiashara wadogo  ambao wamekuwa wakitumia baadhi ya vifungashio vya plastiki kwenye bidhaa wanazouza kwa kuangalia mpango mbadala na kuboresha baadhi ya vibebeo ambavyo havitakuwa na madhara kwenye mazingira.

"Bwana Kayombo hii jaribuni mkae na kulitazama vizuri hasa utoaji wa elimu kwa wananchi,nakubali kuna baadhi ya vibebeo havistahili kama vifungashio kwenye pilipili au vitunguu lakini bidhaa kama Njegere ili imvutie mnunuzi ikiwemo kwenye kibebeo cha kuonekana ana uhakika wa biashara yake kutoka  maana wafanyabiashara hawa wengi mitaji yao ni midogo hawana ubavu wa kuweka bidhaa zao kwenye vyombo maalum ",Mhe.Malima.

Aidha Mhe.Malima ameliahidi Baraza hilo la Mazingira kushirikiana nalo akiwashirikisha viongozi wa Kamati ya Amani Mkoani Mwanza kuzifanyia ukaguzi na kuchukua hatua baadhi ya nyumba za ibada zisizo na sifa na kugeuka kero kwa wananchi.

"Tupo hapa Mwanza kwa muda wa siku saba kufanya ukaguzi kwa wanaokiuka matumizi ya mifuko ya Plastiki na Kelele sumbufu,tunashirikiana na kamati ya ulinzi na usalama wale wote watakaobanika mkondo wa Sheria utawapitia ikiwemo kufunga  kumbi za starehe na nyumba za ibada na kuwachukulia hatua kali ikiwemo kifungo,"Hamad Taimour,Meneja uzingatiaji Sheria NEMC

"Nimefurahishwa na Mhe.Malima kutuletea hapa ukumbini uthibitisho wa matumizi yenye usahihi na usio sahihi wa hivi vibebeo vya plastiki,sisi kama NEMC hii changamoto tumeiona na tutaifanyia kazi lengo ni kuhakikisha mazingira yetu yanabaki salama kwa faida yetu na vizazi vijavyo, bidhaa zote ambazo haziozi ardhini kuhakikisha hazitumiki",Jerome Kayombo,Meneja Kanda NEMC

Baraza la Taifa la Hifadhi ya usimamizi wa Mazingira Tanzania NEMC, lilipitisha sheria ya katazo la matumizi ya mifuko yote ya Plastiki mwaka 2019 baada ya kubainika inachangia kwa kiasi kikubwa uchafuzi na uharibifu wa Mazingira.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti