• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Ofisi ya Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza yatoa Elimu ya Kipindupindu kwa Wanahabari

Posted on: January 16th, 2024

Ofisi ya Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza yatoa Elimu ya Kipindupindu kwa Wanahabari


Ofisi ya Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na Wizara ya Afya zimeendelea na Mkakati wa kudhibiti Mlipuko wa ugongwa wa Kipindupindu ambapo leo wametoa elimu kwa vyombo vya habari.

Akizungumzia utoaji huo wa elimu uliofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya mganga Mkuu wa Mkoa, mtaalamu wa elimu ya afya kwa umma kutoka Wizara ya afya Dkt. Emmanuel Mnkeni amesema jamii inahitaji kupata uelewa wa kutosha namna ya kuuepuka ugonjwa huo,dalili za mgonjwa na njia za kuudhibiti.

"Leo tupo hapa na vyombo vya habari kwa lengo la kuwajengea uwezo tukitambua umuhimu wa kalamu yao kwa jamii,kila mmoja akiwajibika kuweka mazingira katika hali ya usafi hasa vyoo mlipuko wa ugonjwa huu utatoweka," Dkt.Mnkeni

Amesema Kipindupindu kinatibika endapo mgonjwa atafikishwa mapema kwenye vituo vya afya mara baada ya dalili zote kubainika ambapo dalili kuu ni kuhara maji maji yanayofanana na yale ya kuoshea mchele.

"Ndugu zangu wana habari tujikite vyema katika kuelimisha jamii  wakati mwingine wanaingiwa na taharuki bila sababu kama watakosa msingi mzuri wa elimu kuhusiana na ugonjwa huo," Leonard Charles,mratibu elimu kwa umma Ofisi ya RMO

"Tunashukuru kwa kupatiwa elimu hii,ushauri wetu kwa Serikali mamlaka zote husika ziwajibike ipasavyo kwani bado maeneo mengi miundombinu ya maji taka ni mibovu,"Wellington Masele,ITV

Grace Mbise kutoka Star Tv amebainisha bado baadhi ya makabila yanaendeleza mila zisizo na mashiko kwa kutochangia choo wenyewe kwa wenyewe kwa imani za kuepuka mikosi ndani ya familia na badala yake wanakwenda kujisaidia vichakani

"Tunapotumia maji ya visima tunatakiwa kuweka vidonge viwili vya  Water Guard tofauti na maji ya bombani ambayo yanakuwa yamefanyiwa utaratibu wa kitaalamu kutoka kwenye vyanzo na unalazimika kuweka kidonge kimoja lakini tuzingatie kuchemsha maji hadi yatokote,"amefafanua Yusuph Seif Afisa afya kutoka Wizara ya afya.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti