• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RAIS SAMIA MGENI RASMI TAMASHA LA BULABO, RC MAKALLA AWAALIKA WANANCHI KUMPOKEA

Posted on: June 8th, 2023

RAIS SAMIA MGENI RASMI TAMASHA LA BULABO, RC MAKALLA AWAALIKA WANANCHI KUMPOKEA


*Rais Samia kugagua Miradi ya kimkakati*


*Awataka viongozi kujiandaa na ugeni*


*Awakumbusha wakuu wa taasisi kutoa huduma bora*


Mkuu wa Mkoa wa Kwanza Mhe. CPA. Amos Makalla amewataka Wakuu wa taasisi na wananchi kujitokeza kwa wingi kumpokea Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye atawasili Juni 12, 2023 kwa ajili ya uzinduzi wa tamasha la Bulabo pamoja na kutembelea Miradi ya kimkakati iliyopo  Mkoani Mwanza.

Mhe.CPA Makalla amesema hayo leo Juni 8, 2023 kwenye kikao kazi na Wakuu wa Taasisi zinazofanya kazi Mkoani Mwanza ambacho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kikiwa na lengo la kupokea taarifa mbali mbali za miradi inayotekelezwa na taasisi hizo.

"Niwaombe Wakuu wa Taasisi pamoja  wananchi wote wa mkoa wa mwanza kujitokeza kwa wingi katika kumpokea Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye tarehe 12, Juni 2023 atawasili Mkoani hapa na tarehe 13, Juni 2023 atakwenda kwenye uzinduzi wa tamasha la Bulabo na tarehe 14, Juni 2023 atatembelea miradi ya kimkakati," Amesema  Mhe. Makalla


"Naomba kila Mkuu wa Taasisi auone ugeni huu kuwa ni ugeni wetu hivyo tunakila sababu ya kutoa ushirikiano kwa Mkuu wa Mkoa katika kutoa taarifa na ushirikiano wa hali na mali." Ameongeza Mhe. CPA Makalla.

Aidha, Mhe. Makalla ametoa rai kwa Wakuu hao wa Taasisi  kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi ili kusaidia mkoa kuwa katika hali ya usalama.


"Niwaombe muitumie ofisi yangu vizuri katika kuhakikisha tunatoa huduma bora kwa wananchi na hali ya ulinzi na usalama inakua shwari, wote tunategemeana katika kuhakikisha tunatoa huduma bora," Ameongeza CPA Makalla.

"Mimi  Mkuu wa Mkoa ni kiongozi wa shughuli zote  katika Mkoa huu nawaomba ushirikiano katika kutimiza majukumu tuliyopewa na Mhe. Rais,"Mhe. Mkuu wa Mkoa.


Pia, Mhe.Makalla ameitaka Bodi ya Pamba ikifikia msimu ujao wa maandalizi ya kulima na kuuza pamba changamoto zote zilizo ainishwa katika uwasilishaji  zifanyiwe kazi  ili msimu utakapoanza ziwe zimekwisha.

Naye, Mhandisi Paschal Ambros Meneja wa Tanroad Mkoani Mwanza amesema miradi wa kimkakati wa ujenzi wa  daraja la JP Magufuli Lenye urefu wa kilomita 3 ukikamilika itainua maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika Mkoa kwakuwa litaunganisha Wilaya za Misungwi na Sengerema,  ambazo zimetenganishwa na ziwa.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti