• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RAS Balandya ahimiza umakini wa kuwapata Watumishi wenye Weledi

Posted on: April 24th, 2023


Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Bw. Balandya Elikana  amewataka madiwani na wawakilishi kutoka mikoa mbali mbali ya Tanzania  kuwa huru kutoa maoni yao kuhusiana na uboreshaji wa  kanuni za ajira.

 Hayo yamesemwa leo Aprili 24 2023 kwa niaba yake na Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Mwanza Utawala na Rasilimali Watu Bw. Daniel Machunda wakati akifungua semina ya mchakato wa ajira katika utumishi wa umma na ukusanyaji wa maoni kwa ajili ya kuboresha kanuni za uendeshaji wa shughuli za sekretarieti,amewataka washiriki husika kuzingatia kile watakachojifunza ili wakachangie ufanisi wa kazi kwa kupata Watumishi wenye weledi.

Sekretari ya Ajira katika Utumishi wa Umma imeandaa semina hiyo ili kuhakikisha sheria, kanuni, taratibu na miongozo yote ya ajira inazingatiwa ikiwa hichi ndicho chombo kilichopewa mamlaka kisheria kuwezesha upatikanaji wa watumishi katika utumishi wa umma.

"Sekretarieti ya ajira imeona ni jambo zuri  kuwashirikisha na nyinyi wadau ili muwe huru kutoa maoni yenu ambayo yatapelekea kupata kanuni mpya zitakazo ongeza tija katika mchakato wa ajira". Amesema Bw. Machunda

Pia Bw. Machunda amewataka washiriki wa semina hiyo kuzingatia mafunzo yatakayotolewa na wawezeshaji ili iwe rahisi kwao kushiriki kikamilifu katika utoaji wa maoni  ambayo yataboresha kanuni.

Aidha naye Naibu Katibu wa Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma Mhandisi. Samweli Tanguye amesema wameandaa semina hiyo kwa ajili ya kujielezea kwa wadau jinsi wanavyoendesha amichakato ya ajira na kanuni wanazozitumia.

" Tupo hapa Mwanza kwa ajili ya kutoa elimu na kujielezea kwa wadau wetu juu michakato ya ajira inavyoendeshwa na kuwaonesha michakato  ya ajira na kanuni tunazozitumia ili na wao waweze kupata nafasi ya kutoa maoni yao". Amesema Mhandisi. Tanguye

Naye Diwani wa kata ya Bujora halmashauri ya wilaya ya Magu Mhe. Bunyanyakei John amesema  Sekretarieti ya Ajira ikiyafanyia kazi maoni ya washiriki  yataleta matokeo makubwa sana katika ajira.

"Kama sekretarieti ya ajira ikisimamia kweli maoni ya washiriki basi maoni hayo ambayo tutayatoa yataleta matokeo makubwa katika ajira". Amesema Mhe. John

Semina hiyo ya siku mbili inayofanyika ukumbi wa Maji House Jijini Mwanza, imewahusisha Madiwani, Wakuu wa Idara ya Rasilimali Watu kutoka Taasisi za Serikali na wawakilishi kutoka Ofisi za Wakuu wa Mikoa ya Mwanza, Tabora, Geita, Shinyanga, Simiyu, Mara na kigoma.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti