• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RAS BALANDYA AONGOZA KIKAO CHA WATUMISHI, ASISITIZA USHIRIKIANO KUBORESHA KAZI.

Posted on: December 28th, 2023

RAS BALANDYA AONGOZA KIKAO CHA WATUMISHI, ASISITIZA USHIRIKIANO KUBORESHA KAZI


Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Balandya  Elikana leo Disemba 28, 2023 ameongoza kikao cha watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo ambapo pamoja na mambo mengine amewapongeza kwa kazi na amewataka kuendelea kushirikiana katika kufanikisha shughuli za kila siku za kuhudumia wananchi.

Amesema katika kufanikisha hayo kila mmoja anapaswa kuhakikisha anajitoa kwa moyo wa upendo kuhudumia wananchi kwenye eneo lake na kuhakikisha aonapo changamoto anaifikisha sehemu husika kwa ajili ya kuzitatua na kuhakikisha kunakua na ufanisi kwa kufanyia maboresho kwenye eneo husika.

Balandya ameongeza kuwa katika kuhakikisha kuna usalama wa taarifa na uwasilishaji wa haraka na ufanisi wa mafaili ni lazima kutumia mfumo wa Mawasiliano wa Ofisi ambao unafikisha taarifa kwa mhusika na kwamba ofisi yake ipo kwenye mpango mahsusi wa kuboresha suala la vitendea kazi kama ununuzi wa magari ya Idara kadiri bajeti itakavyoruhusu.

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi (TUGHE) tawi la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ndugu, Mangabe Mnilago amewataka watumishi kuendelea kujibidiisha kwenye kazi na Ofisi kuhakikisha wanatatua changamoto za Kimfumo ili kuhakikisha fedha zinapatikana kwa wakati na kufanikisha kusonga mbele kwa kazi.

Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Utawala na Rasilimali watu Ndugu, Daniel Machunda amewashukuru watumishi kwa kujituma na amebainisha kuwa Ofisi yake haina masuala mazito ya kinidhamu na ametumia wasaa huo kuwataka watumishi  kuwahi kazini ili kuhakikisha wanatimiza malengo ya siku katika kuboresha kazi.

Katika nyakati tofauti, watumishi wamewasilisha ombi la kununuliwa Basi ili kurahisisha uendeshaji wa shughuli zinazohitaji watumishi kwenda kwenye kazi kwa makundi kwani kwa sasa Mkoa umekua ukiazima usafiri kwenye taasisi zingine mathalani Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Mei Mosi.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti