• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RAS BALANDYA ATAKA AFUA ZAIDI ULINZI NA USALAMA KWA WATOTO WA KIUME KAMA ILIVYO KWA WA KIKE

Posted on: July 12th, 2024

RAS BALANDYA ATAKA AFUA ZAIDI ULINZI NA USALAMA KWA WATOTO WA KIUME KAMA ILIVYO KWA WA KIKE


Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bw. Balandya Elikana amewasihi watumishi na wadau wa afya mkoani humo kuhamasisha na kuongeza jitihada za kulinda watoto wa  kiume dhidi ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kwa kuongeza zaidi afua zinazolenga kundi hilo kama ilivyo kwa watoto wa kike.

Amesema hayo Julai 11, 2024 alipotembelewa na timu inayofanya ufuatiliaji wa afua za mradi wa DREAMS unaotekelezwa katika kata 18 kwa wanafunzi waliopo shuleni (shule za msingi 73) unaolenga kusaidia binti balehe na wanawake vijana wenye umri wa miaka (15 – 24) wasiosoma (out of school) wilayani  Nyamagana.

"Ni furaha yangu kubwa kuona timu inayofanya ufuatiliaji wa ubora wa takwimu za mradi wa DREAMS unaotekelezwa na Serikali pamoja na wadau wetu ICAP na ELCT/ KKKT wilayani Nyamagana, takwimu zinapokua sahihi na zenye ubora ndipo tunaweza kupanga mipango yenye tija ya kutatua changamoto zilizopo.

Aidha, Katibu Tawala Balandya amesisitiza kufanya usimamizi shirikishi mara kwa mara kwa walengwa ili kufuatilia maendeleo yao na kutatua changamoto zao na kuhakikisha ustawi bora wa jamii.

Aidha, ametumia wasaa huo kutoa ombi kwa wadau hao kwa wakati mwingine kuona namna ya kuwahusisha watoto wa kiume waliopo shuleni na nje ya mifumo rasmi ya elimu ili nao waweze kunufaika na programu za DREAMS kwani nao wapo kwenye hatari ya maambukizi hayo hususani nyakati hizi za wimbi kubwa la ukatili wa kijinsia.

Ameongeza kuwa mradi huo umelenga kuwaibua mabinti zaidi 13,000 ndani ya mwaka wa mradi (OCT 23-SEP 24) kutoa huduma ya upimaji na ushauri nasaha kwa mabinti kutambua sehemu salama ambazo mabinti wanajifunza masomo na uendeshaji wa vipindi na elimu mbalimbali za kujiinua kiuchumi.

"DREAMS (in school) - Inayotekelezwa na mdau wetu- KKKT kupitia mradi wa USAID kizazi hodari kanda ya kaskazini mashariki imeweza kuwafikia mabinti 11,546 (99%) katika lengo la mwaka  (FY2024 ) kufikia mabinti 11,572 katika shule 73 ambazo ziko katika mpango huo ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Nyamagana." Amefafanua Bw. Balandya.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti