• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RAS BALANDYA ATAKA MIKAKATI KUINUA UFAULU WA WANAFUNZI MAGU

Posted on: June 17th, 2025

RAS BALANDYA ATAKA MIKAKATI KUINUA UFAULU WA WANAFUNZI MAGU


Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Ndugu Balandya Elikana ameitaka Menejimenti ya halmashauri ya Magu kuja na mpango wa kufuta ufaulu wa daraja la nne na sifuri kwa wanafunzi ili kuhakikisha dhamira ya serikali ya kuboresha elimu inafikiwa kwa wanafunzi kupata daraja la kwanza.

Ndugu Balandya ametoa maagizo hayo leo tarehe 17 juni, 2025 wakati akiongoza baraza maalum la hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kwa halmashauri hiyo kuishia juni 30, 2024 kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa na kubaini ufanisi usioridhisha kwa shule za sekondari na msingi kwa kipindi cha 2021-2023.

"Elimu ndio msingi wa mbeleni, menejimenti ya Magu tafadhali sana daraja sifuri halikubaliki kwa watoto wetu naomba tukajifunze kwenye halmashauri zingine wanafanyaje kuinua ufaulu mathalani Kwimba twendeni tuone wao wamewezaje kwani mazingira yetu hayatofautiani." Amesema Balandya.

Ameongeza kuwa wazazi na walezi wana wajibu wa kuwafundisha stadi za maisha watoto wao kama kufanya usafi wa mazingira na miili yao ili kuwafanya wawe na utayari wa kujibidiisha na kujenga tabia ya kujitegemea kwani tabia bwete husababisha hata kufeli kwenye masomo.

Aidha, amewaagiza Halmashauri ya wilaya ya Magu kuzingatia mahitaji wakati wa uagizaji wa dawa za binadamu kwa ajili ya kusambaza kwenye vituo vya kutolea huduma ili kuepusha kuisha kwa muda wa matumizi na kulazimika kuteketeza.

Amesema ni hasara kuwa na madawa ya zaidi ya milioni tano yaliyoisha muda wake na kulazimika kuteketeza kwani ni uharibifu wa rasilimali fedha na akaliagiza baraza hilo kufuatilia vibali vya kuteketeza dawa hizo ili zisilete madhara kwa watumiaji.


"Hoja zote ambazo hazijatekelezwa ziwekewe mkakati wa utekelezaji wake ili ziweze kufungwa hivyo naagiza muweke vielelezo na viambatanisho vyote ndani ya muda ili kuifanya halmashauri ibaki salama." Amesisitiza Katibu Tawala.


Naye, Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Nje Mkoa wa Mwanza ndugu Henry Chausa amebainisha kuwa 2023/24 halmashauri hiyo ilikaguliwa na kupata hati inayoridhisha na kwamba kuna hoja 46 ambazo zinafanyiwa kazi na kufungwa.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti