• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RAS BALANDYA ATOA MAAGIZO KWA BARAZA LA MADIWANI UKEREWE USIMAMIZI WA HALMASHAURI

Posted on: June 17th, 2025

RAS BALANDYA ATOA MAAGIZO KWA BARAZA LA MADIWANI UKEREWE USIMAMIZI WA HALMASHAURI


Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Ndugu Balandya Elikana ametoa maagizo kadhaa kwa baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe ikiwemo kusimamia Halmashauri hiyo kwa uzalendo ili kuwasaidia wananchi hususan kwenye matumizi ya fedha za umma.

Ametoa maagizo hayo mapema leo juni 17, 2025 kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa katika Baraza Maalum la kupitia hoja na taarifa ya utekelezaji wa mapendekezo ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kwa halmashauri ya wilaya hiyo kwa mwaka 2023/24 lililofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo mjini Nansio.

Aidha, Ndugu Balandya ameitaka Halmashauri hiyo kuendelea kujibu hoja za Mkaguzi na kuendelea kushirikiana na Ofisi hiyo kwa kuwa Halmashauri inaye Mkaguzi wa ndani hivyo amewataka kumtumia Mkaguzi huyo ili aisaidie Halmashauri kuweza kujifahamu hali zao kabla Mkaguzi wa nje hajafika.

Kuhusu hoja ya utumiaji usioridhisha wa mfumo wa usimamizi wa mali za serikali (GAMIS), Katibu Tawala ameagiza halmashauri hiyo ndani ya kipindi cha robo ya kwanza kutumia wataalamu kutoka Sekretarieti ya Mkoa kuwajengea uwezo wataalam wa ugavi ndani ya halmashauri hiyo ili kumaliza tatizo.

Mkuu wa wilaya hiyo Mhe. Christopher Ndubiagai ametumia baraza hilo kuwakumbusha wajumbe wa baraza hilo kusimamia makusanyo na matumizi ya fedha za umma kwa masilahi ya wananchi wa Ukerewe na akawaalika kushiriki ziara ya Mhe. Rais atakayoifanya juni 19-21 Mkoani humo.

Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Nje Mkoa wa Mwanza ndugu Henry Chausa amebainisha kuwa kwa mwaka wa 2023/24 halmashauri ya wilaya ya Ukerewe ilifanyiwa ukaguzi kwa hesabu na kupata hati inayoridhisha na kwa miaka mitatu mfululizo imeendelea kupata hati inayoridhisha.

"Hoja za miaka ya nyuma halmashauri ilikua na mapendekezo 18 na baada ya uhakiki 16 zipo kwenye hatua za utekelezaji na 2 bado hazijafanyiwa kazi pamoja na agizo 1 la LAAC kutokana na kukosekana na kukosa vielelezo na mkakati wa CMT kujibu hoja." Amesema Chausa.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti