• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RAS Balandya awakumbusha Mafundi Sanifu kufanya kazi kwa uadilifu

Posted on: May 4th, 2023



Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Balandya Elikana amewataka mafundi sanifu kuendelea kufanya kazi kwa juhudi na maarifa lakini pia wawe waadilifu ili waweze kutekeleza miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali kwa kiwango kilichokusudiwa.

Akizungumza kwenye mkutano mkuu wa tano wa mwaka wa mafundi sanifu uliowakutanisha washiriki zaidi ya 500 kutoka mikoa mbalimbali nchini unaofanyika jijini hapa kuanzia leo Mei 4 hadi 5,2023,  Elikana amesema miradi yote inayotekelezwa na serikali  kuna mchango mkubwa wa mafundi sanifu ambao wanaiwezesha kuendelea hivyo ni vyema wakawa waadilifu katika kutimiza majukumu yao.

“Naipongeza sana serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan  kwa kazi kubwa inayofanya ya kuwaletea wananchi maendeleo,  katika mkoa  wetu wa Mwanza tumekuwa tukipokea mabilioni ya shilingi kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati ya maendeleo.

“Tuna miradi ya kimkakati ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa daraja la JPM Kigongo- Busisi, reli ya kisasa, ujenzi wa meli mpya kubwa ya aina yake katika ukanda wa maziwa makuu MV MWANZA HAPA KAZI TU stendi ya mabasi ya abiria Nyegezi na mingine mingi inayotekelezwa na Tanroads na Tarura na hivi juzi tumesaini mkataba kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kilomita 54 kutoka Sengerema hadi Buchosa yote hii tunawategemea nyie mafundi sanifu,” amesema Elikana na kuongeza

“Ni matumaini yetu  miradi hiyo itakapokamilika itachochea sana ukuaji wa uchumi wa mkoa wetu, kanda ya ziwa na nchi kwa ujumla, tunaishukuru sana serikali lakini pia tunawategemea nyie mafundi sanifu mfanye kazi kwa bidii na muwe waadilifu ili tuweze kuitekeleza miradi hiyo na ionyeshe thamani halisi ya fedha,”ameeleza Elikana.

Katika hatua nyingine Katibu Tawala huyo wa Mkoa wa Mwanza aliwasihi washiriki wote wa mkutano huo kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo mkoani humo kabla hawajaondoka.

“Mkoa wetu wa Mwanza umejaliwa kuwa na vivutio vya aina mbalimbali na vya kipekee vya utalii ikiwa ni pamoja na fukwe nzuri zilizopo katika ziwa Viktoria, utalii wa majini, hifadhi ya taifa ya kisiwa cha saa nane na vivutio vya utalii vya utamaduni vilivyopo katika makumbusho ya utamaduni ya wasukuma buchosa,”amefafanua na kuongeza

“Pia Mkoa wetu wa Mwanza umezungukwa na visiwa, Wilaya ya Ukerewe tu inavisiwa takribani 38 visiwa vya ukerewe vina mambo mengi mazuri, kuna kisiwa  cha ukara ambacho kina jiwe linalocheza,”amebainisha Katibu Tawala Elikana.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi kwenye mkutano huo Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi sekta ya Miundombinu, Balozi Mhandisi Aisha Salim Amour ameielekeza Bodi ya Usajili wa Wahandisi nchini(ERB)kupeleka serikalini mpango mkakati utakaotatua changamoto za uhaba wa mafundi sanifu ikiwa ni pamoja na kuboresha mfumo wa elimu na ajira.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti