• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RAS Balandya awapa Rai Madaktari waliopata mafunzo maalum kwenda kuyafanyia kazi

Posted on: May 26th, 2023



Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ndg. Balandya Elikana amewataka washiriki wa  mafunzo ya tathmini ya  ulemavu kwa ajali na magonjwa yatokanayo na kazi  kutumia vyema mafunzo waliyopatiwa na kuyafanyia kazi kwa vitendo.

Amesema hayo leo Mei 26, 2023 wakati akifunga mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Mfuko wa Bima kwa Wafanyakazi (WCF) yaliyo wahusisha Madaktari 100 kutoka katika Mikoa ya kanda ya Ziwa ambayo yamefanyika Mkoani Kwanza.

"Nipende kutoa rai kwa washiriki wote kutumia vyema elimu iliyotolewa katika mafunzo haya ili kuwawezesha kufanya tathmini ya ulemavu kwa ufanisi na weledi wa hali ya juu na hatimaye kuwasadia wanaopata ulemavu unaotokana na ajali au magonjwa yatokanayo na kazi na kuusaidia mfumo wa fidia kwa wafanyakazi kutimiza lengo la kutoa fidia stahiki na kwa wakati," amesema Mtendaji huyo wa Mkoa

"Nchi yetu na Dunia kwa ujumla imekumbwa na mabadiliko ya tabia nchi kutokana na uharibifu wa mazingira kwa msingi huo ni wajibu wa kila mmoja wetu kutunza na kuhifadhi mazingira yetu, tuchukue hatua za makusudi za kuhakikisha kuwa mazingira yetu yanalindwa ikiwemo kulinda vyanzo vya maji, misitu, na kuendelea na zoezi la upandaji miti katika maeneo yetu," ameongeza Ndg. Balandya.

Aidha Mkurugenzi wa Huduma na Tathmini wa (WCF) Dkt. Abdulsalaam Omar amesema mafunzo hayo kwa Madaktari yanakusudia kuusadia mfuko katika kufahamu asilimia za ulemavu na kutoa fidia stahiki na kwa wakati.

" Mafunzo haya yamejikita katika kuwawezesha madaktari kuweza kufanya tathmini lengo kwa ujumla ni kuongeza ufanisi wa kazi na kutoa huduma bora," amesema Dkt. Omar.

Naye Dkt. Paskalet Jumba mshiriki wa mafunzo kutoka Hospitali ya Rufaa Geita  amewasihi washiriki wenzie kwenda kuyafanyia kazi mafunzo waliyopatiwa pia  wanakwenda kuwaelemisha na wengine waliobaki katika vituo vya kazi ili waweze kuielewa elimu hiyo.

Mafunzo hayo  yameendeshwa kwa muda wa siku 5 ambayo yalifunguliwa Mei 22, 2023 na mpaka sasa Madaktari 1585 kwa Nchi nzima wamekwisha kupatiwa elimu hiyo.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti