• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RAS Mwanza afanya ukaguzi wa miradi ya afya isiyokamilika Sengerema,ataka taarifa ya mchakato wa ukamilishaji wiki hii

Posted on: December 19th, 2023

RAS Mwanza afanya ukaguzi wa miradi ya afya isiyokamilika Sengerema,ataka taarifa ya mchakato wa ukamilishaji wiki hii


Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Ndg. Balandya Elikana ametoa maagizo ya kupatiwa  taarifa  ndani ya siku mbili kuhusu mchakato wa ukamilishaji wa miradi 17  ya afya wilayani Sengerema iliyojengwa kwa nguvu ya wananchi ili hatua za haraka zifanyike wananchi wapate huduma.

Akizungumza jana jumatatu na watendaji wa Halmashauri ya hiyo baada ya kufanya ukaguzi wa miradi iliyo kwenye vijiji tofauti, Balandya ameagiza kupatiwa gharama za umaliziaji zikiwemo na nyumba za watumishi na upatikanaji wa vifaa tiba.

"Mkurugenzi nimeona miradi ya zahanati imeishia hatua ya boma,

kaa na timu yako ya wataalamu mfanye kazi hii kwa umakini na taarifa niipate Ofisini kwangu  kabla ya jumatano ili ifanyiwe kazi ngazi husika," amesema Balandya wakati akiwa kijiji cha Nyamasale iliyopo zahanati iliyoishia hatua ya boma.

Akiwa kwenye kijiji cha Nyitundu iliyopo zahanati inayotoa huduma lakini inakabiliwa na uhaba wa vifaa tiba,nyumba za watumishi na wafanyakazi, Mtendaji huyo wa mkoa amemtaka Mkurugenzi kupatia ufumbuzi haraka wa changamoto hizo ili wananchi wapate huduma bora.

Balandya akiwa kwenye ukaguzi huo kijiji cha Tabaruka ameshuhudia  mradi wa zahanati uliofikia hatua ya ujenzi asilimia 38 huku zahanati ya kijiji cha Itonga ikitoa huduma lakini ikikabiliwa na uhaba wa maji na choo hakijakamilika, hapo ametoa agizo la kuchimbwa kisima haraka na ukamilishaji wa choo.

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza imechukua hatua hiyo ikiwa ni utekekezaji wa maagizo ya Waziri wa nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa baada ya kufanya ukaguzi wa baadhi ya miradi hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita na kubaini mapungufu kadhaa, hata hivyo taarifa ya miradi 17 ya afya aliyopatiwa na mbunge wa Sengerema Mhe. Hamis Tabasamu kuwa imekamilika lakini haitoi huduma haikuwa sahihi baada ya Katibu Tawala wa mkoa kubaini miradi hiyo bado ipo hatua ya awali kabisa.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti