• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RAS Mwanza ataka matokeo chanya afya ya Mama na Mtoto

Posted on: February 1st, 2023


Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Balandya Elikana amewataka watendaji wa Afya kuhakikisha wanalinda afya ya mama na mtoto kwa kusimamia vifaa vya kujifungulia na kuhakikisha vinakuwepo vituoni muda wote, ikiwa ni pamoja na uimarishaji wa mfumo wa kumfuatilia mama mjamzito sambamba na maandalizi ya kujifungua.


Bwana Elikana  ameyasema hayo wakati akizungumza katika kikao cha Robo Mwaka cha watendaji wa Sekta ya Afya kwa ajili ya kujadili Vifo vya mama vinavyotokana na uzazi pamoja na vifo vya watoto wachanga kilichofanyika katika Wilaya ya Misungwi.

"Simamieni vifaa vya kujifungulia viwepo vituoni muda wote, Serikali imeendelea kutoa fedha za dawa na vifaa tiba kupitia MSD," amesena Elikana.

Aidha, amesisitiza kuwa asingependa kusikia mama au mtoto amekosa huduma kwa kisingizio cha kukosa dawa, na kutoa angalizo kuwa, mojawapo ya vipaumbele vya Serikali kupitia Sekta ya Afya kwa mwaka 2023 ni ubora wa huduma.

Pamoja na msisitizo wa huduma bora za afya Bw.Elikana amewataka watendaji kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu Bima ya Afya kwa wote na kusimamia utekelezaji ili elimu ya Bima ya Afya itolewe kwa wananchi kupitia vituo vya kutolea huduma za afya na katika mikusanyiko kadri inavyowezekana.

"Hili ni eneo la kipaumbele kwa Serikali linalolenga kuondoa kizingiti cha kutokuwa na fedha kwa wananchi katika kupata huduma ya Afya,"amesisitiza Elikana.

Kwa upande wake Mganga  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Thomas Rutachunzibwa amebainisha wamepokea maelekezo ya Katibu Tawala na kuanza kuyafanyia kazi na wamejipanga imara kuhakikisha Sekta ya Afya inazidi kuwa na matokeo chanya kwa kuzingatia uwepo wa vifaa tiba na huduma bora.

Hata hivyo Bw. Elikana amewakumbusha kuwa Majengo yaliyoelekezwa kujengwa yakamilishwe na yaanze kutumika mara moja, RMO na DMO wahakikishe wanasimamia ili vituo vikamilike kwa wakati,visajiliwe na vianze kutoka huduma kwa wananchi kwani Serikali imewekeza fedha nyingi katika huduma za afya.

 Katibu Tawala amewapongeza Sekta ya  Afya kwa utaratibu wa kufanya vikao kama hivyo vya kujadili changamoto za Kiafya zinazozikabili jamii.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti