• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC MAKALLA AAGIZA KUREJESHWA HALMASHAURI KAMPUNI YA MISUNGWI CO. LTD

Posted on: June 21st, 2023
  1. RC MAKALLA AAGIZA KUREJESHWA HALMASHAURI KAMPUNI YA MISUNGWI CO. LTD


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos Makalla amemuagiza Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi na Idara ya Mipango kuhakikisha wanafanya Marekebisho ya Mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) ili kuhakikisha Kampuni ya Misungwi Company Ltd inamilikiwa na Halmashauri kwa asilimia 100.

Akizungumza kwa niaba yake leo tarehe 21 Juni, 2023 Katibu Tawala Mkoa Ndugu Balandya Elikana wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani Maalum la Kujadili Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa Mwaka wa fedha 2021/22 amesema haiwezekani Kampuni ya Serikali ikaanzishwa na kuendeshwa kwa kukiuka taratibu za umiliki wa Makampuni ikiwemo Mkurugeni wa Halmashauri kuwa Mbia binafsi.

Vilevile, ameiagiza TAKUKURU ndani ya siku 30 kufanya uchunguzi ili kubaini uendeshwaji wa Kampuni hiyo iliyoanzishwa kwa hati ya Usajili Na 140457876 Novemba 21, 2019 ikiwa na Mali za TZS 35,547,983 na fedha Taslimu TZS 24,547,983 na thamani ya Mashine TZS 11,000,000 huku ikiwa na udhaifu kwenye Muundo na Usimamizi na kukosekana kwa gawio la moja kwa moja kwa Halmashauri hiyo.

Aidha, Elikana ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kupata Hati safi na amewataka kuwa na Mwenendo wa kushughulikia Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu kwa haraka ili kujihakikishia wanaendelea kupata Hati safi na kwamba hilo linawezekana endapo watafuata taratibu na Kanuni za Mapato na matumizi ya  Fedha za umma.

Akiwasilisha taarifa kwa niaba ya Mkurugenzi, Mweke Hazina wa Halmashauri hiyo Ngugu Joseph Mazito amesema pamoja na kupata Hati Safi Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali katika mwaka 2021/22 alitoa hoja 16 ambazo zilitakiwa kujibiwa na kuwasilisha majibu kwa ajili ya uhakiki

"Hadi kufikia tarehe ya kikao hiki majibu ya hoja hizo yaliwasilishwa na kuhakikiwa na hoja zilizotekelezwa na kufungwa ni 12 sawa na asilimia 75 huku hoja zinazoendelea kutekelezwa zikiwa ni 4 sawa na Asilimia 25 ambapo jitihada zinaendendelea kuhakikisha zinajibiwa." ameeleza Mwekahazina.

Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Nje Mkoa wa Mwanza, Waziri Shaban ameipogeza Halmashauri ya wilaya ya Misungwi kwa kupata Hati safi na akabainisha kuwa wamekua na mwenendo wa kupata Hati Safi kwa zaidi ya miaka 3 mfululizo na ametoa wito kwa watendaji kuheshimu taratibu za fedha.

"Tunawapongeza Halmashauri ya wilaya ya Misungwi kwani kwa Mwaka wa fedha 2021/22 Halmashauri hiyo ilikaguliwa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na imepata Hati safi huku wakiwa na Agizo moja tu la LAAC ambalo hawajalitekeleza na kuonesha juhudi za kuitekeleza" amesema Ndugu  Waziri Shaban.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti