• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC MAKALLA AFURAHISHWA NA MWENENDO MZURI WA PAMBA JIJI FC, AWAMWAGIA MINOTI

Posted on: January 26th, 2024

RC MAKALLA AFURAHISHWA NA MWENENDO MZURI WA PAMBA JIJI FC, AWAMWAGIA MINOTI


*Awajaza Shs Milioni 5 kama motisha ya kuiangamiza Biashara FC*


*Atangaza tarehe 3 Februari 2024 kuwepo Harambee ya kuichangia Pamba Jiji FC*


*Awahimiza kukaza buti uwanjani kutimiza malengo ya kucheza Ligi kuu msimu ujao*


Leo Januari 26, 2024 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.CPA Amos Makalla amefanya mkutano wa kawaida na wachezaji na timu ya soka ya Pamba Jiji FC na kuwakabidhi kibunda cha Milioni 5 kama motisha ya kuendelea kutoa dozi dimbani katika michezo yake ya Ligi ya Championship.


Mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi yake ulioambatana na chai ya pamoja, Makalalla ambaye pia ni mlezi wa timu hiyo amebainisha amezidi kukunwa na kiwango cha timu hiyo na muendelezo wa ushindi katika michezo yao.

"Mimi ugonjwa wangu ni mpira wa miguu mkinifurahisha katika eneo hili nanyi mtaona matunda yake,hongereni sana kwa kiwango kizuri mlichoonesha katika mpambano wenu dhidi ya Stendi Utd". Mkuu wa mkoa

Amesema mchezo ujao dhidi ya Biashara United kutoka Mara hana shaka ya kushuhudia pointi nyingine 3 zikiendelea kuvunwa na kuzidi kujiimarisha nafasi ya juu katika msimo wa Ligi hiyo.

"Niliwaleta wachezaji 5 kutoka Congo DRC kwa majaribio lakini mwisho wa siku wote hawakuonesha kiwango cha kulishawishi dawati la ufundi kuwasajili,lakini nyie baadhi yenu tuliowaongeza dirisha dogo mpo vizuri hongereni",amesisitiza mlezi huyo aliyecheza pia soka miaka ya nyuma.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema ili kuhakikisha wana TP Lindanda wanazidi kuwa tishio mwanzoni mwa mwezi ujao ataandaa harambee ya kuichangia timu hiyo lengo ni kuzidi kuwapa hamasa na motisha wachezaji hao ili kutimiza malengo ya kucheza Ligi kuu msimu ujao.

Amezidi kuwakumbusha wananchi wa Mwanza kuendelea kushikamana na kuwapa ari wachezaji wa Pamba Jiji FC kwa kujitokeza kwa wingi dimbani katika michezo yake ya nyumbani na hata ugenini


"Hiki unachokifanya Mhe.Mkuu wa Mkoa hata mimi unanirahisishia kazi yangu yaani inakuwa nyepesi kutokana na wachezaji ari ya kujituma na kuyashika maelekezo ya kiufundi inakuwa nzuri,"Mbwana Makatta,kocha wa Pamba Jiji FC


Katika msimamo wa Ligi ya Championship wana TP Lindanda wanashikilia nafasi ya pili na mtaji wa pointi 40 kibindoni.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti