• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC Makalla akabidhiwa rasmi Ofisi,amshukuru Rais Samia kwa kumuamini na kuahidi kuchapa kazi kwa uaminifu na bidii

Posted on: May 28th, 2023

*RC Makalla akabidhiwa rasmi Ofisi,amshukuru Rais Samia kwa kumuamini na kuahidi kuchapa kazi kwa uaminifu na bidii*


 *Awaahidi wana Mwanza kasi ya Maendeleo kwa kushinda Site na *kusikiliza kero zao*


 *Kulivalia njuga tatizo la Maji*


 *Apania Mwanza kuwa na timu ya Ligi Kuu ya NBC*



Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Amos Makalla amekabidhiwa rasmi Ofisi kutoka kwa mtangulizi wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe.Adam Malima na kuahidi kuyatekeleza kwa bidii na uaminifu matarajio yote ya Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kuwaletea maendeleo wananchi  na kuinua kwa ujumla uchumi wa Mkoa huo.

Akizungumza leo kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na viongozi waandamizi wa Serikali, Taasisi na wawakilishi kutoka makundi mbalimbali,Mhe Makalla amesema anatambua amekuja kwenye Mkoa ambao unahitaji kuwa na kiongozi wa mfano katika  kuwatumikia wananchi na kuitekeleza kwa vitendo Ilani ya Chama cha Mapinduzi.

"Mimi siyo mtu wa kukaa Ofisini,muda wote napenda kushinda Site huko ndiyo nitapata kujua ukweli wote wa kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi,nitaanza ziara ya kutembelea Wilaya zote kuanzia tarehe 31 2023",Amesisitiza CPA Makalla.

Aidha kuhusu kero ya maji kwa wananchi wa Mwanza hasa wanaoishi maeneo ya milimani na kwingineko,Mkuu huyo wa Mkoa ameahidi kulivalia njuga suala hilo kwani ana uzoefu wa kutosha alipokuwa Naibu Waziri wa Maji, hivyo ameomba ushirikiano wa dhati kutoka kwa Taasisi husika ili kumaliza kero hiyo.

Kuhusu miradi yote ya kimkakati iliyopo Mkoani humo Mhe.Makalla amebainisha ataitembelea na kuhakikisha inamalizika kwa wakati na kuwa na tija kwa wananchi.

"Ziara yangu nitakayoanza hivi karibuni nataka kuiona miradi yote iliyopo inatekelezeka kwa usahihi na wananchi wanapata maendeleo kwa haraka na nitawapa nafasi wananchi kusikiliza kero zao kama ilani ya CCM inavyotaka ",Mhe.Makalla

Mkuu huyo wa Mkoa wa Mwanza ambaye pia ni mkereketwa wa michezo amesema haoni sababu ya Mkoa huo kukosa timu ya kucheza Ligi kuu ya NBC kutokana na nguvu ya kiuchumi iliyonayo,hivyo atahakikisha anakusanya nguvu za Wadau ili kufanikisha malengo hayo.

Awali akisoma taarifa ya Mkoa ,Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe.Adam Malima amesema bado Mkoa wa Mwanza unakabiliwa na Changamoto mbalimbali ikiwemo kero ya maji,uhaba wa fedha za kukamilisha huduma za jengo jipya la wagonjwa wa Saratani Bugando kutokana na wingi wa wagonjwa wanaotoka Kanda ya ziwa,uharibifu wa Mazingira,na ubadhilifu wa fedha za mikopo kwa makundi maalum kutoka kwenye Halmashauri.

"Mhe.Makalla nakuwachia mambo manne ambayo ni vyema ukaanza nayo,jengo la uwanja wa ndege bado halina ubora kama kweli tunahitaji kukuza soko la utalii,Mgodi wa Madini wa Nyazaga wapo katika hatua ya kuwalipa fidia wananchi umakini unahitajika katika zoezi hili,Zao la Pamba ambalo ni uti wa mgongo kwa Mkoa wa Mwanza bado halimnufaishi Mkulima,Wafugaji Mwanza wanafikia idadi ya 50,000 lakini bado mifugo yao haina tija licha ya Serikali kuwekeza fedha nyingi Sekta ya Kilimo na Mifugo",RC Malima.

Katika hafla hiyo fupi ya makabidhiano ya Ofisi imeambatana na utoaji wa zawadi mbalimbali alizokabidhiwa Mhe.Malima zikiwemo picha za matukio kadhaa aliyoshiriki akiwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, ikiwemo kampeni ya Mkoa huo ya upandaji miti Milioni 23.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti