• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC MAKALLA AMALIZA MGOGORO WA ENEO LA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI NYAMPULUKANO- SENGEREMA

Posted on: November 9th, 2023

RC MAKALLA AMALIZA MGOGORO WA ENEO LA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI NYAMPULUKANO- SENGEREMA


*Aaagiza ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Nyampulukano uanze kwa kasi kwani Serikali imetoa fedha Milioni 200*


*Aagiza pia shule mpya ya SEQUIP ujenzi uendelee haraka*


*Aagiza Mwezi Januari shule zote mpya zitakazojengwa zianze kutoa huduma*


*Awataka watendaji na viongozi kushirikiana  kuchapa kazi na kusahau msuguano wa nyuma*


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos Makalla amemaliza rasmi mgogoro uliodumu kwa zaidi ya miezi sita wa wapi ujenzi wa shule mpya ya Sekondari chini ya Mradi wa Uboreshaji wa Elimu (SEQUIP) wapi ijengwe.

Mhe. Makalla ametatua mgogoro huo wakati akiongea na wananchi wa kata ya Nyampulukano eneo la FDC mlimani ambapo kabla ya kufika hapo alitembelea maeneo yote mawili yaliyopendekezwa kujengwa kwa shule hiyo mpya ya SEQUIP.

Mkuu wa mkoa amesema, kutokana na mgogoro huo kudumu kwa muda mrefu, Serikali ya awamu ya sita imeona ni vyema kujenga shule mpya katika maeneo yote mawili ya Misheni na Nyampulukano ili huduma hiyo muhimu iwafikie wote.

"Serikali imetoa shilingi milioni 200 kwa ajili ya kukamilisha Miundombinu ya madarasa iliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi wakati huohuo shule mpya ya SEQIP itaendelea kujengwa katika eneo lililopendekezwa la kata ya Nyampulukano." Makalla.

Vilevile, amewataka Halmashauri ya wilaya ya sengerema kuongeza kasi ya ujenzi wa shule hizo na kwa pamoja ifikapo mwezi Januari mwakani zianze kutoa huduma kwa wananchi kwani wamesubiri kwa muda mrefu.

"Mimi kama Mtendaji mkuu nakusbukuru sana Mhe. Mkuu wa mkoa maana tulishakwama kutokana na sintofahamu ya wapi tutajenga shule pamoja na kupokea fedha za ujenzi huo, nakuahidi mwezi Januari shule hii itaanza na sasa tunafanya kazi kwa kasi", amesema Mkurugenzi Mtendaji, Binuru Shekidele.

Naye, Diwani kata ya Misheni Mhe. Francis Majumba amefafanua kuwa wananchi wa kata hiyo imepata faraja kutokana na kutatuliwa kwa kitendawili hicho na kupatikana kwa suluhu ambayo inakuja kuwatatulia adha ya kusuasua kwenye maendeleo kwenye eneo la Elimu.

Mapema asubuhi Mkuu wa Mkoa aliliagiza Shirika la Umeme wilaya Sengerema (TANESCO) kupeleka umeme kwenye shule mpya ya msingi ya Kijiweni iliyojengwa kwa zaidi ya shilingi Milioni 540 kwenye kata ya Chifunfu ambayo inakuja kuondoa kero ya msongamano wa wanafunzi kwenye shule mama ya Bugumbikiso.

Vilevile, amemtaka Mkandarasi anayejenga jengo la makao makuu ya Halmashauri ya Sengerema kukamilisha ujenzi huo ifikapo mwezi Mei 2024 kwa mujibu wa mkataba ili huduma zianze kutolewa hapo.

Halikadhalika, amewakaribisha wananchi wa wilaya hiyo kupata huduma za afya zinazotolewa kwenye hospitali mpya ya wilaya hiyo iliyojengwa kwa zaidi ya Bilioni 2.8 na ameahidi kuwasiliana na mamlaka husika ili ziletwe Bilioni 1.5 za kukamilisha ujenzi kwenye hospitali hiyo.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti