• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC MAKALLA ATEMBELEA MIRADI, AHIMIZA IKAMILIKE KWA WAKATI

Posted on: June 16th, 2023

RC MAKALLA ATEMBELEA MIRADI, AHIMIZA IKAMILIKE KWA WAKATI


*Aitaka Halmshauri ya Jiji kuweka mazingira ya muingiliano wa watu soko la Wafanyabiashara wadogo*


*Awakumbusha kuheshimu taratibu zilizowekwa na Serikali za kutengewa maeneo maalum*


*Stendi kuu ya Mabasi Nyegezi kufunguliwa na Rais Samia*


*Aahidi kusimamia Mradi wa Maji ukamilike kwa wakati wananchi waondokane na kero ya maji*



Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos Makalla leo Juni 16, 2023 amekagua Miradi  ya Soko la Machinga la MchafuKoga, Stendi kuu ya mabasi Nyegezi na mradi wa Maji Butimba Wilayani Nyamagana na kutaka miradi hiyo ikamilike kwa wakati ili kuleta tija ya wananchi.

Akianzia soko la Mchafu Koga linalojengwa kwa gharama ya zaidi ya Shs. bilioni 1.4 ameutaka uongozi wa Jiji la Mwanza kuhakikisha wanafanya shughuli zao katika mazingira rafiki yenye muingiliano wa watu ili wajihakikishie wateja.

"Nimesikia taarifa yenu ya ujenzi wa soko hili, lakini mtambue siyo tu kujenga soko zuri bali mzingatie kufikiwa na wananchi kiurahisi ikiwemo mabasi kupita maeneo haya ili watembea kwa miguu wazione bidhaa kirahisi," CPA Makalla.

Amewakumbusha pia wafanyabiashara hao ndogo ndogo kuendelea kuheshimu taratibu zilizowekwa na Serikali za kutengewa maeneo yao maalum na siyo kukimbilia kupanga bidhaa zao barabarani.

Akisoma taarifa ya mradi wa ujenzi wa soko kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Edward Mwamotela amesema ili kuendeleza ujenzi wa Block B na C Halamashauri imepokea Shilingi Bilioni 9 kwa mwaka wa fedha 2022-2023 kutoka mradi wa Green and Smart Cities na kwa mwaka wa fedha ujao 2023-2024 imetengwa bajeti ya shilingi Bilioni 1 kutoka mapato ya ndani.

"Uongozi wa Wilaya na Mkurugenzi kaeni na wadau wote waliopo hapa stendi ili mzisikilize changamoto zilizopo hapa na mzishughulikie na msikilize ushauri wao juu ya namna ya kuendesha standi ili kutoka na mapendekezo mazuri," amesema Mhe. CPA. Makalla.

Amesema wakati Stendi hiyo ya mabasi iliyokamilika kwa asilimia 100 na kuwa katika majaribio kero zote zitatuliwe na atamuomba Rais Mhe.Dkt.Samia Suluhu kuja kuifungua rasmi.

"Ujenzi wa stendi ya Nyegezi umekamilika kwa asilimia 99.5 na kazi zilizobaki ni kufunga Mageti na  Stendi imeanza kufanya kazi tarehe 5, Juni 2023, Stendi ya Nyegezi ina eneo la kuegeshea mabasi 120 na magari madogo 80 kwa wakati mmoja,"amesema  Edward Mwatomola, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji.

Akikagua mradi wa maji wa Butimba uliogharimu Shs. bilioni 69 na kutarajiwa kuukamilishwa na kukabidhi kwa Serikali Julai 30 mwaka huu na Mkandarasi SOGEA SATTON kutoka Ufaransa, Makalla amesema atausimamia kidete kuhakikisha makubaliano ya makabidhiano yanafanyika kama ilivyopangwa ili wananchi waondokane na tatizo la maji.

Halamashauri ya Jiji la  Mwanza ni miongoni mwa Halmashauri ambazo zinatekeleza miradi ya kimkakati ambayo inalenga kuziwezesha Halmashauri nchini  kuongeza mapato na kupunguza utegemezi kwa Serikali kuu.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti