• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC MAKALLA AZITAKA HALMASHAURI ZA ILEMELA NA JIJI KUANDAA MPANGO WA KUBORESHA MAPATO YA STENDI ZA NYAMHONGOLO NA NYEGEZI

Posted on: June 26th, 2023

RC MAKALLA AZITAKA HALMASHAURI ZA ILEMELA NA JIJI KUANDAA MPANGO WA KUBORESHA MAPATO YA STENDI ZA NYAMHONGOLO NA NYEGEZI


*Amewataka Kukutana na LATRA na TABOA kwa ajili ya ufanisi*


*Awataka wapitie upya bei ya vyumba katika Stendi hizo*


Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. CPA. Amos Makalla amezitaka Halmashauri za Manispaa ya Ilemela na Jiji la Mwanza kuandaa mpango kazi wa kuboresha mapato ya Stendi za Nyamhongolo na Nyegezi na kujifunza kutoka katika Halmashauri zingine ambazo zimefanikiwa kupitia vyanzo hivyo vya mapato.

Mhe. CPA. Makalla amesema hayo wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kwa ajili ya kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) za Mwaka 2021/22 leo Juni 26, 2023.

"Angalieni vyanzo vya mapato mlivyo navyo ili mpate ushuru, wekeni huduma stahiki katika vyanzo hivyo ili muweze kuwashawishi watu Kwa vile vyanzo ambavyo vinatoa mapato navyo msimamie  boresheni huduma katika masoko katika stendi ili kuhakikisha mapato yanapatikana" CPA Makalla.

"Mkae muweke mkakati wa kuboresha mje na mpango kazi mzuri ndio maana nikatoa nafasi mwende mkajifunze kutoka kwenye majiji na Halmashauri ambazo zina stendi kama yenu, muwaangalie wanafanikisha vipi katika ufanisi wa stendi ili tujifunze katika manispaa zilizofanikiwa katika kuziendesha hizo stendi" amesisitiza Mkuu huyo wa Mkoa

Aidha, Mhe. Makalla  ameitaka Menejimenti ya Halmashauri hiyo kuhakikisha wanajibu hoja zote za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ili kuhakikisha Halmashauri inaendelea kupata hati safi.


"Leo tumekaa hapa kujadili hoja hizi  ni kazi ya menejimenti mkurugenzi ukasimamie kuhakikisha hoja hizi zinatekelezwa na fanyieni kazi jibuni hoja zote kama ambavyo imeelekezwa na pale mtakapokwama msipate tabu ya namna ya kuwasiliana na ofisi ya CAG ili kupata namna ya kuziondoaha hizo hoja.


Naye, Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Nje wa Mkoa wa Mwanza, Waziri Shabani kwa niaba ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali amesema kwa hesabu zinazoishia tarehe 30 Juni 2022  Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela ilipata hati inayoridhisha.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti