RC Malima achangia milioni 20 timu zinazoshiriki Championship Mwanza

Timu za ligi ya Championship kutoka mkoa wa Mwanza (Gwambina FC, Copco Veteran FC na Pamba FC) zimetakiwa kuhakikisha zinainua vipaji na kuviendeleza ili kukuza mchezo wa mpira wa miguu.
Hayo yamesemwa leo Oktoba 25, 2022 na Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Malima wakati alipozungumza na wadau wa soka katika mkoani humo.
‘’Timu zetu zinatakiwa kuwa na vipaji na kuhakikisha zinaendeleza, hivyo vipaji ili viweze kufika katika timu zetu za Taifa Stars,’’ amesema Malima.
Amezitaka timu za Copco Veteran, Gwambina FC na Pamba FC kupambana ili Mkoa wa Mwanza uweze kupata timu itakayoweza kupanda ligi kuu kwa msimu ujao.
Amesema katika timu zote tatu kwa sasa kila timu inahitaji kusaidiwa katika mipango ya kifedha na amebainisha kuwa yeye atatoa Shilingi milioni 20 kwajili ya kuzisaidia timu hizo ziweze kufanya vyema.
Aidha, ametoa rai kwa timu hizo kutengeneza mfuko malumu kwa ajili ya kuzisaidia katika mashindano ya ligi ya championship na kwenye hilo ni lazima kuwe na mkakati wa kuhakikisha zinatumika inavyotakiwa.