• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC Malima aipongeza Serikali kwa kuboresha huduma Sekta ya afya

Posted on: May 6th, 2023


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Malima amesema ni muhimu kuimarisha njia za upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi  ili kuhakikisha   huduma bora kwa wananchi zinatolewa kwenye vituo vya afya nchi nzuma

Hayo yamesemwa leo Mei 6 2023 na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ndg. Balandya Elikana kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kuhusu mfumo mpya wa mshitiri  katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa.

"Ni muhimu sana kuimarisha upatikanaji wa dawa, vifaa tiba, vifaa saidizi na vitendanishi kulingana na mahitaji ya vituo vya afya katika ngazi zote za utoaji huduma nchini  na kuhakikisha  huduma bora zinatolewa kwa wananchi," Amesema Mtendaji huyo wa Mkoa

Ndg. Balandya ameipongeza  Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambao ndio wawezeshaji wa mafunzo hayo kwa kuendelea kuboresha mfumo wa mshitiri na endapo utasimamiwa vizuri utasadia upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi.

" Niipongeze Ofisi ya Rais - TAMISEMI kwa kuendelea kuboresha mfumo wa mshitiri na ni matumaini yangu na Serikali kuwa mfumo huu endapo utasimamiwa vizuri utasaidia  katika upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi zinazokosekana katika Bohari la Dawa," Amesema Ndg. Balandya.

Aidha  Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Claudia Kaluli amesema  Ofisi ya Rais- TAMISEMI  ikishirikiana na wizara ya afya imeleta mfumo wa uagizaji dawa ambazo zitakua hazipatikani katika Bohari la Dawa ambao ni rahisi.

" Ofisi ya Rais- TAMISEMI  ikishirikiana na wizara ya afya imeleta mfumo wa uagizaji dawa ambazo zitakuwa zinakosena katika Bohari la Dawa  ambao ni rahisi na utasaidia kuweza kushirikiana na wauzaji binafsi,"  Amesema  Kaluli

"Huu ni mfumo ambao tunaimani unakuja kuleta mageuzi chanya kwenye Sekta yetu ya afya kutokana na upatikanaji wa haraka wa dawa na usahihi wa nyaraka husika",Julius Shigella,Mratibu wa huduma za Maabara na damu salama Mkoa.

Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2023  iliweka bayana na kawaahidi wananchi kuimarisha mifumo ya upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi  na kuimarisha ushirikiano na sekta binafsi katika utoaji wa huduma za afya.

Washiriki wa mafunzo hayo ni Wakurugenzi kutoka Halmashauri zote za Mkoa wa Mwanza,Waganga wakuu wa Wilaya,Maafisa TEHAMA,waratibu wa huduma za Maabara na Maafisa ugavi.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti