• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC Malima akipongeza Chama cha Madaktari wa tiba za Wanyama kwa kutoa elimu hiyo kwa wanafunzi wa kike Mwanza

Posted on: April 29th, 2023


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Adam Malima amekipongeza Chama cha Madaktari wa Tiba za Wanyama nchini TVA kwa kuyatumia Maadhimisho ya Kitaifa Mwanza ya siku ya utoaji huduma za afya ya wanyama, kwa kutoa elimu shuleni kuwahamasisha wanafunzi wa kike kuchangamkia taaluma hiyo.

Akizungumza kwa niaba yake leo wakati wa ufungaji wa Maadhimisho hayo kwenye viwanja vya Furahisha,Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mhe.Hassan Masala amesema kumekuwa na kasumba ya mfumo dume kuwa kazi hiyo ni ya wanaume kutokana na kuwakabili wanyama wengine wenye ukali na nguvu,jambo ambalo halina ukweli wowote.

"Tumemshuhudia Rais wetu Mhe.Dkt.Samia Suluhu akiweka mazingira mazuri ya kuwepo na shule maalum za wasichana  kuchukua masomo ya Sayansi,hii maana yake ni kutaka kuwepo na uwiano mzuri wa wataalamu wa kike wa kulijenga Taifa letu".Amesema Mkuu huyo wa Wilaya.

Amewakumbusha pia wakazi wa Mwanza wenye mifugo kuyachangamkia Maadhimisho hayo kwa kupata elimu ya kutosha na kuona umuhimu wa chanjo za mara kwa mara za mifugo yao ili iwe  salama kwa mlaji na uhakika wa soko.

"Ndugu mgeni rasmi mbali ya kuhamasisha elimu hiyo shuleni,April 27 tumetoa huduma mbalimbali za mifugo bila malipo zikiwemo chanjo na upasuaji na kufikisha idadi ya mifugo 607 tuliyohudumia siku hiyo maeneo ya Kisesa wilayani Magu,lengo likiwa ni kuwaelimisha wananchi kuwa na mifugo bora wakati wote,"James Kawamala,Katibu wa TVA Taifa.


"Maadhimisho haya Kitaifa tumeyafanya kwa mara ya kwanza na tukachagua Mkoa Mwanza ambao una sifa ya kuwa na wafugaji wengi,hivyo tumefarijika elimu tuliyotoa itakuwa na tija kwao na Taifa kwa ujumla," Prof.Esron Karimuribo,mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Kila ifikapo wiki ya mwisho ya April,Tanzania hujumuika na Mataifa mengine Duniani kuadhimisha siku ya utoaji huduma za afya ya wanyama ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni Kukuza utofauti,usawa na ushirikishwaji katika taaluma ya tiba ya wanyama.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti