• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC Malima asaini Mkataba wa Lishe baina yake na Wakuu wa Wilaya za Mwanza

Posted on: October 28th, 2022

*RC Malima asaini Mkataba wa lishe baina yake na Wahe.Wakuu wa Wilaya*


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Adam Malima leo Octoba 28 ameongoza zoezi la utiaji saini wa Mikataba ya Afua za Lishe  baina yake na Wahe. Wakuu wa Wilaya saba zilizopo mkoani humo.

Akizungumza kabla ya kutia saini mikataba hiyo, Mhe.Malima amewataka Wahe.Wakuu wa Wilaya hizo  kuhakikisha wanaisoma na kuielewa ili waweze kuifanyia kazi kikamilifu kama ambavyo imekusudiwa na Serikali.

" Nawaombeni Wahe. Wakuu wa Wilaya  isomeni na kuielewa siyo kuisoma tu kwa kuwa mkiielewa mtaifanyia kazi na matokeo tutayaona ila mkiisoma tu mtaiacha hapo hapo," amesema Mhe.Malima.

" Chakula cha Lishe hakitakiwi kuwa na gharama kubwa... sasa nawaambia Wahe.Wakuu wa Wilaya nendeni mkatoe Elimu ya Lishe ....na haina haja ya kutumia maneno magumu waelewesheni wananchi kwamba lishe siyo lazima iwe mayai, nyama na samaki wambieni  lishe ni mboga za majani kama matembele, kunde, maharage vyote hivyo ni lishe" amesisitiza Mhe.Malima.

Aidha, ameongeza kuwa  mikataba hiyo inashuka mwanzo ilikuwa kati ya  Mhe.Rais  Samia Suluhu Hassan na Wakuu wa Mikoa na sasa ni Mkuu wa Mkoa na Wahe. Wakuu wa Wilaya na baadaye Wakurugenzi.

Hata hivyo, Mhe.Malima ameongeza kuwa Jambo kubwa katika mikataba ya Lishe ni Elimu juu ya Swala la lishe, kwa kuwa vitu vyote vinavyohusu Lishe vinapatikana katika mazingira ya wananchi.

"Wapeni  Elimu wananchi  juu ya matumizi ya vyakula hivyo ili viwaletee afya watoto wetu,"amesisitiza

Naye, Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt.Thomas Rutachunzibwa amesema mkataba huu ni wa msingi sana ukizingatia kuwa hali ya Udumavu iko juu takriban asilimia 29 katika mkoa wa Mwanza hivyo wameupokea Mkataba huo na kuahidi kuusimamia katika utekelezaji wake.

Kwa upande wake Bw.Daniel Machunda Katibu Tawala Msaidizi Utawala  Mkoa wa Mwanza  akimuwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa huo Balandya Elikana, awali akimkaribisha Mhe.Mkuu wa Mkoa amesema kikao hicho ni kufuatia agizo la Mhe.Rais  Samia Suluhu Hassan kuwa ifikapo Oktoba 30 Mikataba yote ya Lishe iwe imesainiwa.

Kikao hiki kimefanyika kufuatia maelekezo ya kikao kazi yaliyotolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, na Maafisa Lishe walio katika Sekretarieti za Mkoa kilichofanyika Mwezi Septemba, 2022 Mkoani Dodoma kuhusu Afua za Lishe, ambapo Mhe.Rais alielekeza Ofisi ya Rais TAMISEMI Kupitia Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wilaya kusaini mikataba ya Utendaji kuhusu masuala ya Lishe kati ya Mkoa na Halmashauri zao zote.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti