• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC Malima awafafanulia Maafisa wa Majeshi ya Ulinzi kutoka Mataifa mbalimbali fursa za kiuchumi zilizopo Mkoani Mwanza

Posted on: October 10th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Malima amesema Jiji hilo linazidi kukua kiuchumi kutokana na rasilimali zilizopo na kuwa kitovu cha Biashara eneo la Nchi za Maziwa Makuu.

Akizungumza leo kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Maafisa wanafunzi wa Majeshi ya ulinzi wanaosoma Chuo cha ukamanda na unadhimu Duluti Arusha, Mkuu huyo wa Mkoa amesema Uchumi wa bluu unaotokana na Ziwa Victoria umechangia kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na Viwanda kwa ujumla.

Amesema kuondokana na uvuvi wa kawaida unaotumia nguvu nyingi na kupata samaki wachache, sasa wamepiga hatua kwa Wananchi kuelimishwa kutumia uvuvi wa kisasa na Ufugaji Samaki kwenye Vizimba  kwa kufuga kwa muda mfupi na kupata faida kubwa.

"Kwa kutambua Mwanza ni Mkoa wa kimkakati Serikali ya awamu ya Sita imeleta Miradi mingi mikubwa ukiwemo ujenzi wa soko la kisasa la Kimataifa, Ujenzi wa Reli ya kisasa

(SGR) ambayo itarahisisha shughuli za kiuchumi na kufanya uzidi kukua", amesema Mkuu huyo wa Mkoa.

Mhe Malima amesema kutokana na soko zuri la Samaki huko barani Ulaya na shughuli za Utalii, ukarabati wa uwanja wa kisasa na wa kimataifa wa ndege unaendelea ili kuruhusu ndege kubwa za kimataifa za mizigo na abiria kufanya shughuli  zake za kibiashara Mkoani humo.

Awali akizungumzia lengo la ziara yao ya mafunzo Mkoani Mwanza,  Mkuu wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu (CSC) Duruti Brigedia Generali Sylvester Damiani amebainisha wametambua Mkoa huo una mambo mengi ya kujifunza ya kiuchumi na Kijamii pia kupakana na nchi jirani watajifunza mikakati ya kujiimarisha kiulinzi na changamoto zake hivyo siku nne watakazokuwa hapo wataelimika vizuri na kushauri pia.

Aidha, amesema Chuo hicho kinatoa mafunzo ya kijeshi na uongozi ngazi ya Diploma, Degree na Sayansi ya kijeshi kwa Maafisa hao ili kuwaandaa kwenda kushika nyadhifa za juu kwenye majeshi yao.

"Ziara yetu imebeba Kauli mbiu ya Amani na Usalama kwa Maendeleo Endelevu tutapata somo zuri tutakapo kuwa kwenye ziara hii kwenye Wilaya za Ilemela, Nyamagana na Misungwi," amesisitiza Bregedia Generali Damiani.

Mkuu wa Mkoa akijibu swali kutoka kwa Meja Abduwelly Isack kutoka Kenya kuhusiana na mkakati wa Mwanza kuinua zao la Pamba amesema Serikali ya awamu ya Sita imeaimarisha Vyama vyote vya Ushirika ambavyo awali havikusimamia ipasavyo,pili imemuinua mkulima kwa kuboresha bei nzuri ya Pamba, kumpatia mbegu bora pamoja na mbinu za ulimaji wa kisasa.

Meja Lydia Damas kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania ametaka kujua Maendeleo ya Uchumi wa bluu na suala la usalama kwa wavuvi Ziwani, Mhe Malima amesema usalama upo wa kutosha hasa kutokana na kuimarisha doria na kuwashughulikia wachache waliojitokeza kufanya uharamia pia Wananchi wameshirikishwa kutoa ushirikiano kwa vyombo vya usalama wanapotokea watu wenye kutiliwa shaka.

Malima ameongeza kuwa Viwanda na Wananchi wanaendelea kuelimishwa kupitia Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) kuhusu utunzaji wa Ziwa Victoria kuepuka kutiririsha taka ambazo zinakwenda kuua mazalia ya samaki na kuleta madhara kwa afya ya mwananchi kwa ujumla.

Maafisa hao wanafunzi wanatoka nchi marafiki na Tanzania ikiwemo Kenya, Uganda, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Afrika Kusini, Rwanda, Burundi, Msumbiji, Nigeria, India na Misri.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti