• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC Malima awahakikishia wananchi Sengerema ulinzi na usalama miradi ya Barabara na Kivuko

Posted on: April 23rd, 2023


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh.Adam Malima amemshukuru Rais Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuonesha kwa vitendo Miradi ya kuwainua wananchi kiuchumi na kuwaahidi wakazi wa Sengerema ulinzi na usalama wa Miradi iliyosainiwa leo ya Barabara ya Sengerema-Nyehunge ya KM 54.4 na Kivuko cha Buyagu-Mbalika.

Akimkaribisha Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Mhe.Mhandisi Godfrey Kasekenya kwenye hafla ya utiaji saini wa Miradi hiyo kwenye viwanja vya mnadani Wilayani Sengerema,Mhe.Malima amesema hayupo tayari kushuhudia uhujumu uchumi kwenye Miradi hiyo kwa kufanyika udokozi wa aina yoyote wakati Serikali ya Rais Samia ikiwa mstari wa mbele kuwapigania maendeleo wananchi wake.

"Leo tumeshuhudia muendelezo wa miradi mingi hapa Mkoani kwetu,huu wa Barabara umegharimu zaidi ya Shs Bilioni 73 na wa Kivuko zaidi ya Shs Bilioni 3 ni lazima tuoneshe umakini kwenye Miradi hii yenye tija kwa wananchi".Amesisitiza Mkuu huyo wa Mkoa

Aidha amewakumbusha Wakandarasi walioshinda zabuni hizo kuwa na weledi katika kazi zao ziwe na ubora na  kukamalisha kwa wakati miradi hiyo ili kuharakisha maendeleo ya wananchi.

"Nawapongeza sana Wabunge wa Mkoa wa Mwanza,Mhe.Eric Shigongo wa Buchosa,Mhe.Alexander Mnyeti wa Misungwi na Mhe.Hamis Tabasamu wa Sengerema mnafanya kazi kubwa ya kuwapigania maendeleo wananchi wenu hali ambayo nami mnanirahisishia   kwa kiwango kikubwa,asanteni sana".Mhe.Malima.


"Kwa mwaka huu tuna jumla ya Vivuko vipya 6 vilivyo gharimu Sh Bilioni 33.2 na vya ukarabati vipo 18 vilivyogharimu Shs Bilioni27.5,hii inaonesha ni jinsi gani Serikali ya awamu ya Sita ilivyoweka kipaumbele uimarishaji wa miundombinu ambayo ni nguzo muhimu wa uchumi wa nchi"Mhe.Mhandisi Godfrey Kasekenya,Naibu Waziri  wa Ujenzi na Uchukuzi.

Akizungumzia ujenzi wa barabara hiyo Mbunge wa Sengerema Mhe.Hamis Tabasamu amesema kwa muda mrefu shughuli za kiuchumi kuanzia za mazao ya Uvuvi na kilimo zilizorota kutokana na hali mbaya ya miundombinu ya barabara,lakini kwa ujenzi huo sasa utakuwa na tija pia kwa Halmashauri za Sengerema na Buchosa.

"Mheshimiwa Naibu Waziri Kasekenya nakupongeza kwa hatua hii,lakini jimboni kwangu barabara ya Mwanangwa-Misasi hadi Kahama mwaka huu usiponiwekea kiwango cha lami sitakuelewa nimeizungumzia kwa muda mrefu sana kutokana na umuhimu wake."Mhe Alexander Mnyeti Mbunge wa Misungwi.

"Binafsi namshukuru sana Mhe.Rais Jimbo langu asilimia kubwa wakazi wake wapo visiwani,kuimarishiwa barabara hii ni ukombozi kwao hasa katika shughuli zao za Uvuvi kwani watakuwa wanafanya kazi zao kwa uhakika".Mhe.Eric Shigongo,Mbunge wa Buchosa.

Utiaji huo wa saini kwa upande wa barabara umewahusisha Mtendaji Mkuu wa Tanroad nchini Mhandisi Rogatus Mativila na Mkandarasi AVM Construction kutoka Uturuki na upande w Kivuko alikuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa ufundi na umeme TEMESA, Mhandisi Lazaro Kilahala na Mkandarasi Songoro Marine.

Kwa mujibu wa mikataba hiyo Ujenzi wa barabara utachukua muda wa miaka miwili na miezi minne na Kivuko ni miezi kumi.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti