• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC Malima azitaka Asasi za kiraia kushirikiana na Serikali kutokomeza unyanyasaji wa kijinsia

Posted on: March 9th, 2023


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Malima amehimiza Asasi za kiraia ziwe mstari wa mbele kwa kushirikiana na Serikali kuelimisha umma kuhusu kutokomeza unyanyasaji wa kijinsia ili jamii iishi kwa upendo na kujenga Uchumi wa nchi.

Akizungumza Wilayani Kwimba katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yalikofanyika ki mkoa Wilayani humo,Mhe.Malima amesema bado kunahitajika jitihada za kutosha za kuelimisha umma hasa kutokana na matendo ya ukatili kwa Wanawake kuzidi kushamiri hali inayotishia kuja na kizazi kijacho kisicho staarabika.

"Wanawake ni nguzo imara sana katika kuchangia Uchumi wa nchi,na wamekuwa mfano mzuri wa kurejesha mikopo wanayopata kwenye Halmashauri,unapo mtenga mwanamke  kiuchumi,kisiasa au shughuli yoyote ya kijamii hatari yake ni kubwa,"amesema Mhe.Malima.

Aidha, Mhe.Malima amewataka wazazi kujenga utamaduni wa kuwa karibu na watoto wao na kuzungumza nao mara kwa mara hali ambayo itawasaidia kujua mapema mienendo michafu inayowakabili.

"Watoto wengi wamekuwa mbali na wazazi wao kwa kuwaogopa, huku wakikabiliwa na vitendo vichafu hii siyo sawa tubadilike, amesisitiza Mhe. Malima.

"Rais wetu Mhe.Dkt. Samia ameonesha mfano wa mwanamke shupavu wa kupigania maendeleo ya Taifa letu, amewapa na anaendelea kutoa nafasi mbalimbali za uongozi kwa Wanawake,wajibu wenu msimuangushe na badala yake mchape kazi kwa bidii kwa kuiga mfano wake," ameongeza Mhe.Ng'wilabuzu Ludigija Mkuu wa Wilaya ya Kwimba.

"Tusisahau kuwekeza kwenye familia zetu, Serikali ya awamu ya Sita imepania kumuinua mtoto wa kike katika mabadiliko ya teknolojia, zitajengwa Shule maalum za kuwapa kipaumbele wanafunzi wa kike ili wasiwe nyuma katika ulimwengu huu wa Sayansi na Teknolojia, kwa hiyo tusijisahau kuziunga mkono juhudi hizi," amesema Mhe.Anjelina Mabula Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

"Kila ifikapo Maadhimisho haya tuyatumie kujipima  harakati zetu mbalimbali kwa lengo la kusonga mbele katika nyanja mbalimbali ili tufike katika malengo letu tuliyonuia," amesema Mhe.Merry Masanja Naibu Waziri Mali Asili na Utalii.

Katika Maadhimisho hayo wakina mama wajawazito kutoka kata 30 za Wilaya ya Kwimba wamekabidhiwa majiko ya Gesi kwa lengo la kumuondolea  mwanamke adha ya kutumia muda mrefu kusaka kuni.

Kila ifikapo Macho 8 Dunia huadhimisha siku ya Wanawake huku chimbuko lake likiwa ni kukabiliana na vitendo vya unyanyasaji dhidi yao.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti