• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC Malime aagiza aliyeua Albino Kwimba akamatwe haraka

Posted on: November 4th, 2022


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Malima amefika kwenye kijiji cha Ngulla kuwapa pole Bi. Minza Marco (Mjane wa Marehemu), wananchi na wanafamilia kufuatia Kifo cha kikatili cha Ndugu Joseph Mathias (50) kilichotokea usiku wa tarehe 02 Novemba, 2022 baada ya watu wasiojulikana kumkata Mkono wa kulia na kusababisha kifo chake.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ngulla alipofika kijijini hapo kuwapa pole, Malima amewahakikishia famila hiyo kuwa Serikali itahakikisha watuhumiwa waliofanya tukio hilo wanasakwa na kukamatwa popote walipo na watachukuliwa hatua kali za kisheria.

"Hili jambo ni baya sana na limetutia doa hivyo naliagiza jeshi la Polisi na vyonbo vingine ndani ya wiki moja wanieleze ni kitu gani kilitokea hapa maana wanaoamini kwamba unaweza kutengemeza maisha kwa viungo vya watu wengine naamini walishakwisha ila leo imenidhihirishia kwamba bado mambo haya yapo kwenye jamii." Malima.

Aidha, Malima ametoa Tshs. Milioni Moja kwa familia hiyo kama Ubani na amewataka kuwa na subira na Imani katika kipindi hicho kigumu cha huzuni na kwamba mamlaka zinazohusika zinaendelea na uchunguzi wa mwili na ifikapo ijumaa ya tarehe 04, 11, 2022 watakabidhiwa mwili ili kuweza kumzika.

"Hatuwezi kumrudisha mume wake, ila mkono wa sheria utafuata mkondo wake na hatutawaacha wahuni hao na kuruhusu  wakitembea kwenye ardhi ya Mwanza lazima watakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria," asema Malima.

Aidha, ametoa wito kwa wananchi wa Ngulla na vijiji vya jirani kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi na vyombo vingine vinavyohusika na uchunguzi kusaidia kutoa ushahidi wa wanachokifahamu kufuatia jambo hilo ili waliotekeleza wanachukuliwe hatua kali za  kisheria na kulikomesha.

"Ndugu zetu hawa wenye ulemavu wa ngozi wana haki ya kuishi ndani ya Mkoa wa Mwanza bila kubughudhiwa na mtu yeyote na hawa Mabwana (Kamati ya Usalama) wakishindwa kuwapata waliofanya tukio hili nitamwomba Mhe. Rais awaondoe wote maana watakua hawatoshi." Amesisitiza Malima.

Kaimu Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoa ACP Mairi Makori amesema Marehemu amefariki majira ya saa 5 usiku akiwa amelala na mke wake nyumbani kwake kwenye kijiji cha Ngulla ambapo aliitwa na mtu aliyefika nyumbami hapo na na kugonga mlango huku akimwita jina afungue Mlango na alipotoka nje alishambuliwa na kukatwa mkono wa kulia.


Mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye Ulemavu Mkoa, Alfred Kapole ametoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kuua Albino kwani jambo hilo ni baya sana na linatia hofu sana kwa wanachi wenye ulemavu huo na ametoa rai kwa mamlaka husika kuchukua hatua kali za kisheria kwa aliyetekeleza suala hilo.

"Sisi tumeumbwa kwa mfano wa Mungu na wala haijulikani kwamba Mungu alimuumba mtu wa aina gani kwa mara ya kwanza hivyo naomba tumrudie Mungu lakini pia nasi tubaki kuwa salama maana sasa  tutaanza kuomba fedha za kuendesha maisha kwa kuhofia kwenda shambani kulima." Kapole.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti